Thursday, February 10, 2011

KUIONA SIMBA NA ELAN DE MISTSOUDGE ELFU ISHIRINI



Klabu ya SIMBA imesema kuwa wanatarajia kupata ushindi katika mchezo wa marudiano  ya  ligi ya klabu bingwa AFRIKA dhidi ya timu ya ELAN DE MISTSOUDGE ya COMORO mchezo utakaofanyika jumapili wiki hiii huku ikitangaza viingilio vay mchezo huo.

Afisa habari wa SIMBA CLINFORD NDIMBO amesema kuwa wamefanya maandalizi mazuri na kuwataka wapenzi wengi kujitokeza kusingalia timu yao ili iweze kupata hamasa.

NDIMBO ametaja viiingilio vya mchezo  kuwa ni kuanzia shilingi elfu ishirini,elfu kumi na tano,elfu nane na kiiingilio cha chini kikiwa ni shilingi elfu tatu.

Kwa mujibu wa  NDIMBO  waamuzi wa mchezo huo wanatoka nchini RWANDA,a mbapo pia amesema kuwa wachezaji HILARY ECHESA na NIKO NYANGAWA hawatacheza kutokana kuwa majeruhi .

SIMBA inahitaji kupata ushindi wowote ule ili iweze kujihakikihsia nafasi ya kusonga mbele katika mchuano hiyo ambapo ikishinda itakuwa na kazi dhidi ya  klabu  ya TP MAZEMBE ya JAMUHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU