Baraza la Michezo la Taifa BMT limevitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka ya TANZANIA BARA kutoa msukumo zaidi katika dhana ya utawala bora .
Mwenyekiti wa Baraza la hilo hapa nchini Kanali Mstaafu IDD KIPINGU amesema kuna mazoea miongoni mwa vilabu kuweka tatizo la ukosefu wa fedha kama kipaumbele cha kwanza ilihali kinachokosekana katika vilabu hivyo ni utawala bora.
KIPINGU ameyasema hayo alipokuwa akifungua semina ya viongozi wa vilabu inayoendeshwa na FIFA ambapo amesema pia vilabu vya TANZANIA vinahitaji kujifunza masuala mengi zaidi kutoka katika nchi zilizoendelea katika mchezo huo.
Kwa upande wake rais wa shirikisho la soka nchini TFF LEODGER TENGA amesema mpango huu ni makubaliano na shirikisho la soka DUNIANI FIFA kufanya mabadiliko katika soka
Semina hiyo ya FIFA kwa viongozi wa vilabu hapa nchini ina malengo ya kuvifanya vilabu vya TANZANIA viendane na mfumo wa FIFA ambao unavitaka vilabu vijiendeshe kwa njia za kisasa zaidi .
0 maoni:
Post a Comment