Tuesday, March 29, 2011

MOSHA ASEMA HANAMPANGO WA KURUDI YANGA

                                     
           Aliyekuwa makamu mwenyeki wa YANGA DAVIS MOSHA akionyesha kadi yake ya yanga   
                             MOSHA akiongea na waandishi wa habari
Baada ya kuachia ngazi katika klabu ya YANGA aliyekuwa makamu mwenyekiti wa YANGA DAVIS MOSHA amesema licha ya baadhi ya wanachama wa YANGA kumuomba arejee katika klabu hiyo hayuko tayari kwani ameandika barua ya kujihuzulu na baadhi ya viongozi wenzake wamefurahia kuondoka kwake katika klabu hiyo

MOSHA amesema baada ya kuondoka YANGA sasa ananzisha kampuni ambayo atashirilikiana na wadau wengine kutoka nje ili kusaidia yatima kupitia michezo ,amesema kampuni hiyo itakuwa ni kuleta timu kutoka nje akiwemo timu zinazocheza ligi ya ENGLAND ambazo zitakuwa zinacheza mechi na vilabu vya hapa nyumbani na mapato yake yatasaidia watoto yatima

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU