Tuesday, March 15, 2011

TAMASHA LA UZALENDO JUMAMOSI MACHI 26 MWAKA HUU JIJINI DSM

 Kushoto ni RUGE MTAHABA akiwa na mkurugenzi wa GLOBAL PUBLISHERS ERICK SHIGONGO pamoja na mratibu wa tamasha JUMA MBIZO wakiongea na waandishi wa habari juu ya tamasha la uzalendo.

Kampuni ya Global Publishers ikishirikiana na Clouds media group inapenda kuufahamisha umma wa watanzania kuwa wameandaa tamasha la wazi na la bure lillilopewa jina la TAMASHA LA UZALENZO TANZANIA KWANZA SISI SOTE NI NDUGU ,tamasha hilo linatarajia kufanyika jumamosi ya tarehe 26 machi 2011 katika viwanja vya Biafra Kinondoni DSM kuanzia saa 5 asubuhi hidi saa kumi na 12 jioni.

Madhumun i ya tamasha hili ni kuwakumbusha watanzania umuhimu wa kuishi pamoja kwa upendo na amani bila kujali  tofauti zao. Vilevile kuwahamasisha kuipenda nchi yao na kupendana kama binadamu na kuweka uzalendo mbele kwa maslahi ya Taifa, Tamasha ili linakadiriwa kujumuisha watu kati ya 20000 hadi 25000 wa rika tofauti na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa makampuni na taasisi mbalimbali wanaoheshimika na jamii ambao siyo wanasiasa.

Katika tamasha hilo kutakuwa na burudani kutoka bendi mbalimbali na vikundi mbalimbali vya sanaa kati burudani hizo ni AFRICAN STARS, MSONDO MUSIC BAND, DDC MLIMANI  PARK ,TOT BAND na STONE MAYIYASIKA na taarabu pamoja na bongo frava kibao.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU