Timu ya Taifa ya ngumi za ridhaa imeondoka leo kwenda nchini UGANDA kwenda kushiriki mashindano ya majiji yaliyopangwa kuanza April 1 hadi nne mwak huu.
Katibu mkuu wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchini MAKORE MASHAGA amesema timu imeondoka na wachezaji sita wa uzito tofauti wakiwa chini ya kocha MCUBA pamoja na viongozi wa BFT.
MASHAGA amesema wacheza waliondoka ni PATRICK MAXMILIAN, SELEMAN KIDUNDA, VICTOR NJAITI, YAHAYA MALIKI, SAID IDD na ISMAIL IZAK.
Katibu amesema mabondia hao wamechaguliwa kutokana na uwezo wao katika nchumi nidhamu .
Mashindano hayo ya MAJIJI yanashirikisha mabondia kutoka nchini za AFRIKA MASHARIKI NA KATI ikiwemo TANZANIA,KENYA,RWANDA BURUNDI na wenyeji wa mashindano UGANDA.
Mabondia hao wanatarajia kurudi nchini APRIL 5 mara baada ya mashindano kumalizika APRIL 4 mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment