Friday, April 8, 2011

26 WAITWA TWIGA STARS

Kocha wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars), CharlesBoniface ametangaza majina ya wachezaji 26 watakaoanza mazoezi Aprili 11 mwaka
huu kwa ajili ya mechi yao ya mchujo ya michezo ya Afrika (All Africa Games)
dhidi ya Sudan.
 
Wachezaji walioitwa ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Neema Jacob (SimbaQueens), Sophia Mwasikili (Sayari), Fadhila Hamad (Uzuri), Irene Matowo(Mburahati Queens), Hellen Tolla (JKT), Mwanahamisi Shurua (Mburahati Queens),Fatuma Jawadu (Sayari), Fatuma Swalehe (Simba Queens), Maimuna Mkane (JKT),Pulkelia Charaji (Sayari), Fatuma Makusanya (Simba Queens) na Mwanaidi Tamba
(Mburahati Queens).
 
Wengine ni Fridiana Daudi (JKT), Fatuma Salum (Mburahati Queens), MwajumaAbdillah (Tanzanite), Mariam Fakil (Tanzanite), Mwasiti Selemani (Tanzanite),
Aziza Lugendo (Mburahati Queens), Suzana Komba (TMK), Rukia Hamisi (Evergreen),Pendo Juma (Evergreen), Zena Khamis (Mburahati Queens), Tatu Said (UmongaSekondari, Dodoma), Mwanaidi Khamis (Uzuri Queens)  na Zena Said (Uzuri Queens).
 
Kwa siku kumi za kwanza, Twiga Stars itafanya mazoezi Uwanja wa Karume kwawachezaji kutokea nyumbani (off camp) na baada ya hapo itaingia rasmi kambini Aprili 20 mwaka huu.
 
Twiga Stars itacheza mechi yake ya kwanza ugenini Aprili 30 mwaka huu, wakati yamarudiano itachezwa Mei 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.Twiga Stars ikiitoa
Sudan itakuwa imefuzu kwa michezo ya All Africa Games ambayo itafanyika Septembamwaka huu jijini Maputo, Msumbiji.
 
MAPATO AFRICAN LYON v YANGA
.
 
Mechi namba 125 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya African Lyon na Yanga iliyochezwaAprili 7 mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeingiza sh. 22,252,000.


Mapato hayo ni kutokana na watazamaji 4,476 waliolipa kutazama mechi hiyo.
Viingilio katika pambano hilo vilikuwa sh. 15,000 kwa VIP, sh. 8,000 Jukwaa
Kubwa, sh. 5,000 Jukwaa la Kijani n ash. 3,000 Mzunguko.
 
Baada ya kuondoa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh.3,394,372.88 fedha iliyobaki kwa mgawanyo kwa pande zote husika ni sh.
18,857,627.12.
 
Jumla ya gharama za awali za mchezo ni sh. 5,185,200 wakati kila timu ilipatash. 4,101,728.14. Uwanja sh. 1,367,242.71, TFF sh. 1,367,242.71, gharama za
mchezo sh. 1,367,242.71, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 136,724.27, Chamacha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 546,897.08 na Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 683,621.36.

 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU