Sunday, April 3, 2011

MKUTANO MKUU WACHANGIA STARS

Timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo inashiriki michuano ya kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazochezwa Gabon-
Equatorial Guinea mwakani imechangiwa sh. 1,980,000.

Fedha hizo kwa Taifa Stars iliyo kundi D pamoja na Morocco, Algeria na Jamhuri
ya Afrika ya Kati zilichangwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) uliofanyika Machi 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es
Salaam.

Wajumbe wa Mkutano huo walishuhudia mechi kati ya Taifa Stars na Jamhuri ya
Afrika ya Kati iliyochezwa Machi 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Walichanga fedha hizo kuipongeza Stars baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

MAPATO SIMBA v KAGERA SUGAR
Mechi namba 122 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Kagera Sugar iliyochezwa
Machi 29 mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeingiza sh. 23,637,000.

Baada ya kuondoa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh.
3,605,644 fedha iliyobaki kwa mgawanyo kwa pande zote husika ni sh.
20,031,355.93.

Jumla ya gharama za awali za mchezo ni sh. 3,635,600 wakati kila timu ilipata
sh. 4,918,726.78. Uwanja sh. 1,639,575.59, TFF sh. 1,639,575.59, gharama za
mchezo sh. 1,639,575.59, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 163,957.56, Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 655,830.24 na Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 819,787.80.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU