MABINGWA wa Afrika katika mashindano ya ligi ya mabingwa, TP MAZEMBE ya CONGO imewaondosha mabingwa wa TANZANIA, SIMBA katika mashindano hayo ya AFRIKA baada ya kukubali kichapo cha magoli MATATU kwa MAWILI ya SIMBA katika mchezo wa awamu ya pili uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini DSM.
Katika mchezo huo TP MAZEMBE waliweza kutumia vizuri dakika ISHIRINI za awali , kwani mshambuliaji wa timu hiyo GIVEN SINGULUMA alikosa magoli kadhaa katika dakika hizo.
Huku SIMBA nayo ikikosa magoli kadhaa katika dakika hizo kupitia kwa washambulaiji wake kama MUSSA HASSAN MGOSI na MBWANA SAMATTA
Goli la kwanza la timu ya TP MAZEMBE lilifungwa na GIVEN SINGULUMA katika dakika ya KUMI na SITA ya mchezo ya mchezo.
Hadi kipindi TP MAZEMBE ilikuwa ikiongoza kwa goli MOJA.
Kipindi cha pili kilianza ambapo katika dakika ya 58 ya mchezo mchezaji wa SIMBA, SHIJA MKINA aliipachikia goli la kusawazisha timu yake.
Katika dakika ya 63 ya mchezo, ALAIN KALUYITIKA aliipachikia goli la pili timu yake ya TP MAZEMBE.
Katika dakika ya 65 ya mchezo, Simba ikapachika goli lake kupitia kwa mchezaji wake chipukizi MBWANA SAMMATTA, goli ambalo halikudumu kwa muda mrefu kwani ALAIN KALUYITIKA ambaye alipachika goli la TATU kwa timu yake.
SIMBA imetolewa kwa jumla ya magoli SITA kwa MATATU kwani katika mchezo wa awali uliofanyika CONGO timu ya TP MAZEMBE iliichapa SIMBA, magoli MATATU kwa MOJA.
Kwingineko timu za AL AHLY ya MISRI, DEPORTIVO INTERCLUBE ya ANGOLA, ASC LES JARAAFS ya SENEGAL, EL HILALY ya SUDAN na RAJA CLUB ATHLETIC ya MOROCCO nazo zimepata nafasi ya kusonga mbele na mashindano haya barani AFRIKA.
0 maoni:
Post a Comment