Friday, April 15, 2011

TWIGA STARS YAFUZU FAINALI ZA ALL AFRICAN GAMES NCHINI MSUMBIJI

TIMU ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imefuzu kushiriki fainali zijazo za Olimpiki baada ya wapinzani wao, Sudan kujitoa katika mashindano hayo.

Twiga Stars ilikuwa ishuke mechi ya kwanza Aprili 30 huko Sudan na kurejeana na wapinzani wao hao waliojitoa hapa nyumbani Mei 14 hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah, alisema kuwa wamepokea taarifa kutoka katika Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kwamba Sudan haitaweza kushiriki michuano hiyo na hivyo kuipa nafasi Twiga Stars kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza.

Osiah alisema kuwa kutokana na taarifa hizo sasa timu hiyo iliyokuwa imeanza mazoezi chini ya Kocha wake, Mkuu, Boniface Mkwasa, itavunja kambi na baadaye itatafutiwa mechi mbalimbali za kirafiki ili kujiweka imara na michuano hiyo itayoshirikisha timu nane katika hatua hiyo ya fainali.

Sudan nao walifuzu kucheza hatua ya pili baada ya wenzao wa Kenya kujitoa katika hatua ya kwanza kutokana na kutokuwa na timu ya wanawake.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU