U23 KWENDA UGANDA APRILI 14
Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 inatarajia kuagwa (Aprili 14 mwaka huu) saa 7 mchana katika ofisi za TFF kabla ya kuondoka saa mbili baadaye kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya mchujo ya michezo yaAfrika (All Africa Games) itakayochezwa Jumamosi (Aprili 16 mwaka huu)

Msafara wa timu hiyo utakuwa na wachezaji 20 na benchi la ufundi lenye watu sitaukiongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar(ZFA), Hafidh Ally Tahir.
Wachezaji watakaokuwemo katika msafara huo niShaaban Kado, Juma Abdul, David
Luhende, Babu Ally, Shomari Kapombe, Jabir Aziz, Salum Aboubakar, Thomas
Ulimwengu, Mbwana Samata, Kigi Makasi, Gharib Mussa, Mbwana Bakari, Idrisa
Abdulrahim, Innocent Wambura, Khamis Mcha, Awadh Issa, Amour Suleiman, Himid
Mao, Mrisho Ngassa na Salum Telela.
Pia leo mchana (Aprili 13 mwaka huu) timu hiyo imekabidhiwa jumla ya sh. milioni
22 ambazo iliahidiwa endapo ingeitoa Cameroon kwenye michuano ya Olimpiki. Fedha
hizo ziliahidiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya
Simba Trailers.
NSSF kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake Dk. Ramadhan Dau ilikabidhi sh. milioni 10
wakati Azim Dewji ambaye ni Mkurugenzi wa Simba Trailers alikabidhi sh. milioni
12. Kati ya fedha hizo ilizotoa Simba Trailers, sh. milioni 10 ni kwa ajili ya
timu, sh. milioni mbili kwa ajili ya kipa aliyeokoa penalti na wafungaji wa
mabao mawili ya U23.
U23 imepangiwa kucheza na Nigeria katika raundi ya pili ya michuano ya Olimpiki
ambapo mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Juni 4 na 5 mwaka
huu.
0 maoni:
Post a Comment