Thursday, April 28, 2011

WAZIRI MAGUFULI AZINDUA BODI MBILI ZA USHAURI YA WAKALA NA MAJENGO TBA NA TEMESA

 Waziri wa ujenzi JOHN MAGUFULI akisalimiana na mwenyekiti wa bodi za ushauri za TEMESA IDRISA MSHORO
                                              Wakati wa uzinduzi wa bodi za TEMESA na TBA
Waziri wa Ujenzi JOHN MAGUFULI amezindua bodi mbili za ushauri ya wakala wa majengo TBA na bodi ya wakala wa ufundi na umeme TEMESA pamoja na mambo mengine amekeme tabia ya wafanyakazi wa vivuko kuwa na stakabadhi mbili ambazo zinakosesha serikali mapato.

MAGUFULI  pia ameitaka bodi ya ushauri ya wakala ya majengo kujenga nyingi  za gharama nafuu  ili kuwawezesha watumishi waweze kumudu kuzinunua. 

Tatizo la vivuko la linaendele katika katika sehemu mbalimbali ambavyo Tanzania ina vivuko zaidi ya ishirini ambavyo viantegemewa na wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi za TBA na TEMESA waziri wa ujenzi na JOHN MAGUFULI amesema kwa sasa atahakisha watendaji wote wanafanya kazi kwa mujibu na sheria.

Waziri wa Ujenzi JOHN MAGUFULI pia amewataka watendaji wa bodi ya ujenzi kujenga nyumba nyingi za bei nafuu ili kuwawezesha wafanyakazi kumudu nyumba hizo

Zaidi ya nyumba elfu kumi zinatarajiwa kujengwa kwa kipindi cha mwaka huu na tayari nyumba zaidi ya nyumba elfu moja tayari zimeshajengwa.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU