Hakitoa somo kwa wacheza wa shule ya makongo kabla ya kuondoka
ANDY COLE,mshambuliaji wa zamani wa klabu ya MANCHESTER UNITED na ENGLAND jana ameshinda hapa nchini.
Yeye kama balozi wa MAN.UNITED alikuwa na kazi ya kutoa ujuzi wake wa soka kwa vijana chipukizi kupitia mpango wa KUVUMBUA VIPAJI vya SOKA, ARRISING STARS.
Mpango huu unafanywa kwa ushirikiano na MAN.UNITED na kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL.
Na kwa mujibu wa mwakilishi wa MAN.UNITED aliyeambatana na COLE NICK HAMFREY mpango huu kwa sasa umelengwa kwa mashabiki wa MAN.UNITED barani AFRIKA ambao idadi yake inafikia MILIONI 42.
NICK anasema MAN.UNITED itatoa ujuzi wa kiufundi ikiwa ni kutoa makocha ili wawafundishe vijana watakaochaguliwa mbinu bora za soka, na watakapoweza watarejesha AFRIKA ili nao wao wawe chachu ya maendeleo.
Jana ANDY COLE alikuwa kwenye shule ya sekondari ya MAKONGO jijini DSM.





0 maoni:
Post a Comment