Monday, June 20, 2011

TBL KUPITIA BIA YA CASTLE LAGER IMEDHAMINI MASHINDANO YA KAGAME KWA SHILINGI MILIONI MIA TATU

Mkurugenzi wa masoko wa TBL David Minja akimkabidhi mkataba wa  udhamini wa mashindano ya Kagame katibu mkuu wa CECAFA Nicolaus Msonye huku Rais wa CECAFA LEODGER TENGA akishuhudia .TBL imedhamini mashindano hayo kwa shilingi milioni mia tatu ambapo mashindano hayo yanatarajia kuanza Juni 25 hadi Julai 9 mwaka huu katika uwanja wa Taifa Jijini DSM.

Bia ya Castle Lager itadhamini mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Castle Cup yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 25 Juni hadi 9 Julai 2011.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), David Minja alisema “Castle Lager imeona ni wajibu kusaidia mpira wa miguu kwani ndio mchezo maarufu zaidi katika nchi za Afrika Mashariki na Kati. Kagame Castle Cup imetupatia fursa ya kuungana na wanywaji wa Castle Lager kupitia mchezo waupendao.”

Minja aliongeza “Udhamini wetu wa michuano ya Kagame Castle Cup ni muendelezo wa mchango wetu kuendeleza mpira wa miguu ili kuhakikisha Afrika Mashariki inakuwa kinara wa soka barani Afrika kama bia ya Castle Lager ilivyo kinara kwa mauzo, usambazaji na upatikanaji barani Afrika. Udhamini wetu wetu pia utatoa mchango mkubwa kuhakikisha kiwango cha soka la Afrika ya Mashariki na Kati kinakua katika ngazi ya vilabu na timu za taifa ili mataifa yetu yaweze kufuzu kushiriki kombe la dunia mwaka 2014.

“Ikiwa ni bia inayoongoza barani Afrika, Castle Lager inawajibika kuwa mstari wa mbele katika masuala mbalimbali kwa kuzingatia umuhimu wa michuano ya Kagame Castle Cup kwa Tanzania ambayo inasherekea miaka 50 ya uhuru wake, tumeamua kudhamini michuano hii. Uamuzi wetu kujihusisha upya na mpira wa miguu hapa Afrika Mashariki kupitia Kagame Castle Cup utaiwezesha Castle Lager kuendelea kujenga uhusiano na na walaji wake na kuendeleza uhusiano wa muda mrefu na mchezo wa soka barani Afrika”.

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodgar Tenga alitoa shukrani kwa bia ya Castle Lager kudhamini michuano ya Kagame Castle Cup 2011. “Kwa niaba ya wadau wote wa mpira na shirikisho la CECAFA, tunashukuru sana kwa udhamini wa Castle Lager kwa michuano hii,” Tenga alisema. “Mpira wa miguu katika kanda yetu unaendelea kunufaika na misaada ya kifedha,

washabiki wetu wana kiu ya kuona soka la kiwango cha hali ya juu na mafanikio, kupitia msaada huu wa Castle Lager, tutaweza kuandaa mashindano ya ubora wa hali ya juu na kukuza soka katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati. Fedha tunazozipata leo zitaelekezwa kwenye timu ili ziweze kufanya vizuri.”

Castle Lager, bia inayoongoza barani Afrika imedhamini mashindano ya Kagame Castle Cup kwa kiasi cha shilingi milioni 300.

Castle Lager - The Perfect Beer for the Perfect Moment.

ABOUT CASTLE LAGER

Castle Lager has won many local and international awards, including the Grand Champion Award at the Brewing Industry International Awards at Burton-Upon-Trent in England (2000) and the Gold Award at the Australian International Beer Awards (2000).

Country of origin

South Africa

Beer type:

Lager

Alcohol content by volume

5%

Carbohydrates

165 kJ per 100 ml

Taste

It is a standard-strength lager with a special taste, somewhat dry, somewhat bitter, never sweet taste.

Colour

Golden

Availability

It is brewed in 9 countries worldwide but can be found in over 40 countries

Packaging

330 ml bottles and cans, 375ml and 750ml bottles, and 450ml cans.

ABOUT KAGAME CASTLE CUP

The Kagame Castle Cup (CECAFA Club Cup Championship) was officially launched in 1974 in Dar, Tanzania. It is a competition for the champion clubs from 11 member countries of CECAFA. President Paul Kagame of Rwanda became the patron of CECAFA in 1999 and he was honoured by being named after the popular club cup competition since 2002.

The championship is the most popular club cup competition at zonal level in Africa. President Kagame sponsors the prize money to the tune of US 60,000 annually.

The championship will be played over a period of two weeks and the teams will be divided in three groups to play group stage, quarter finals, semi finals, third place match and final.

Teams that have confirmed to participate in this year’s championship include Simba SC and Yanga. The rest are: Ulinzi (Kenya), St. George (Ethiopia), Mereikh (Sudan), Ocean View (Zanzibar), Banamwaya (Uganda), Red Sea (Eritrea), ELman (Somalia), Port FC (Djibouti), APR holders and Eticele (Rwanda) and Vitalo (Burundi).


 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU