Sunday, June 26, 2011

WASICHANA walioshiriki shindano la Urembo Kitongoji cha Chang’ombe, Kanda ya Temeke Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Jumamosi walipata usingizi kwa furaha ya aina yake.
Faraja hiyo ilisababishwa na Mkurugenzi wa Kampuni mpya ya kuibuka vipaji vya wasanii Pappa-Zi, Zacharia Hans-Pop aliyewachafua wasichana hao kwa dola 2,400 za Marekani.

Tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita usiku katika hafla ya kuwapongeza walimbwende hao iliyofanyika Ukumbi wa Club de Silver Pipe-Kawe, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo iliandaliwa na kampuni ya Pappa-Zi ambayo ilidhamini shindano la Miss Chang’ombe lililofanyika Juni 17, mwaka huu kwa wasichana 12 kushiriki.

Pappa-Zi ilianza kwa kumwaga dola 100 kwa kila mrembo aliyeshiriki bila kujali mshindi pamoja na walimu wao wawili, hivyo kufanya fedha ya Mmarekani iliyotolewa kuwa dola 1,4000

Aliyetoa zaidi hiyo ni Mratibu wa shindano hilo, Tom Chilala kabla ya balozi wa Pappa-Z, Jacqueline Wolper kutoa dola 200 kwa mshindi wa tatu, Joyce Maweda na dola 300 kwa mshindi wa pili, Husna Twalib

Baadaye Hans-Pop, mwenyewe akajitokeza na kutopa kitita cha dola 500 kwa mrembo wa taji hilo, Cyncia Kimash ambaye alimrithi Genevive Mpangala ambaye kabla ya kuwa mrembo wa Tanzania, alitokea kitongoji hicho.

Kwa nyakati tofauti, warembo hao walielezea kufurahishwa kwao kwa zawadi walizovuna siku hiyo na kueleza kwamba hiyo ni changamoto ya kufanya vema kwenye mashindano ya kanda na lile taji la mrembo wa Tanzania.

Kwa upande wake, Hans Pop alisema kwamba yeye na kampuni yake wamesukumwa kusapoti mashindano hayo kwa kuwa ni sehemu ya ajira na chimbuko la kupata washiriki wapya wa tasnia ya filamu kwa wale watakaohitaji.

“Unajua kuna hii kampuni yetu ya Pappa-Zi. Kazi yake mbali ya kuibua na kuendeleza vipaji itakuwa ikifanya kazi ya kusambaza nakala ya filamu mpya na bora kutoka kwa wasanii wote…



“Kampuni yetu haitabagua, ila itafanya kazi kwa kuangalia ubora na si kuangalia mtu kama ambavyo inafanywa sasa na kampuni nyingine zinazotaka wasanii fulani wacheze na wao watoe zawadi,” alisema bosi huyo ambaye kampuni yake iko Mikocheni “B” kwa Warioba, jijini Dar es Salaam

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU