Wednesday, August 3, 2011

NGUMI ZA RIDHAA WAPATA MSAADA KUTOKA AIRTEL

Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mkononi wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi T-shirt 100 kwa niaba ya Airtel kusaidia shirikisho la Ngumi Tanzania anaekabidhiwa ni Katibu wa chama cha Waamuzi wa mchezo wa ngumi Taifa Juma Suleiman (katikati). T-shirt hizo zitatumika   katika mashindano ya klabu bingwa ya Ngumi za Ridhaa yanayoendelea sasa mkoani Mwanza kwa kushirikisha vilabu toka mikoa yote na yatafikia kilele siku ya nanenane.wa kwanza kulia pichani ni Makoyo Sangula Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ngumi.






Airtel yasaidia mashindano ya ngumi taifa Tarehe 03 July 2011 Kampuni ya simu za mkononi ya airtel imedhamini mashindano ya club bingwa ya taifa ya michezo ya ngumi za rithaa yanayoendelea mkoani mwanza katika viwanja vya kirumba ambapo yatafikia kilele  siku ya nane nane 8/8/2011.
 
Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Katibu wa chama chama cha waamuzi wa michezo ya ngumi taifa, Juma Suleiman alisema." Tunaishukuru kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kutupatia vifaa hivi vya mazoezi ambazo ni T-shirt zitakazotumika na wachezaji wa vilabu shirika toka mikoa yote wakati wa mashindano.
 
Hii inaonyesha kuwa mnadhamira ya dhati ya kusaidia na kuinua kiwango cha mchezo wa ngumi nchini Mashindano haya ya club bingwa ya taifa yanahusisha timu za mkoa na vilabu mbalimbali  hapa nchini kwa lengo la kujiaandaa na mashindano ya kimataifa ya All African Game yatakayofanyika msumbiji, hivyo basi tunapenda kuwakaribisha wakazi wote wa jiji la mwanza kuona mashindano haya  ni kivutio kikubwa  aliongeza Bw Suleiman Akikabidhi msaada huo.
 
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema Airtel imejipanga katika kuchangia sekta ya michezo nchini, Airtel tunaendelea na mkakati wetu wa kukuza michezo aina yote nchini Tanzania na ndio maana leo hii tunaanza ushirika huu na wana masumbwi Tayari tumejikita katiaka mashindano mpira wa miguu ya U-17 ya Airtel rising star ambayo kwa sasa yamefikia ngazi ya nusu fainali, ni matumani yetu kuwa ushirikiano mzuri kati yetu na wadau wa michezo kama hawa watatuletea michanganuo endelevu ili tuendelee kuwa na wanamichezo bora watakaoitangaza nchi yetu vyema katika mashindano mbali mbali.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU