Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amewaita kwenye kikosi hicho wachezaji Juma Jabu kutoka Simba na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ wa Azam kwa ajili ya mechi ya kirafiki inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Wachezaji hao wameitwa kuchukua nafasi za Amir Maftah wa Simba na Nurdin Bakari wa Yanga ambao ni majeruhi. Mechi ya FIFA dhidi ya Sudan ‘Nile Crocodile’ itafanyika Agosti 10 mwaka huu jijini Khartoum na timu inatarajiwa kuondoka Agosti 8 mwaka huu kwenda huko.
Stars hivi sasa inaendelea na mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi hiyo ambayo ni moja ya maandalizi kabla ya Septemba 3 mwaka huu kuivaa Algeria ‘Desert Warriors’ jijini Dar es Salaam kwenye mechi ya mchujo ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani Gabon na Guinea ya Ikweta.
37 SERENGETI BOYS WAITWA MAZOEZINI
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Kim Poulsen na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo wameita wachezaji 37 kwa ajili ya mazoezi kujiandaa kwa michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Michuano hiyo imepengwa kufanyika Nairobi, Kenya mwishoni mwa mwezi huu ingawa bado CECAFA haijatoa uthibitisho wa kuwepo.
Wachezaji hao wanatakiwa kuanza mazoezi ya asubuhi na jioni kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam siku ya Jumatatu (Agosti 8 mwaka huu).
Walioitwa ni Hamad Hamad (Skaba FC), Aishi Manula (Serengeti Boys), Mwalo Ilunga (Saigon), Mgaya Jafari (Sifa United), Ismail Gambo (Kioma United), Miraji Selemani (Mwere Kids), Mohamed Mohamed (Moro United), Pascal Matagi (Agram), Hussein Ibrahim (Moro), Selemani Bofu (Makongo Sekondari) na Mudathiri Abbas (Orange Academy).
Maulid Mwishere (Kombora), Clever Mkini (Matembe), James Mganda (Morogoro), Mohamed Kharabu (Avizona), Faridi Shah (Amani Centre), Mbwana Hassan (Champion), Idrissa Said (Amana), Michael Mpesa (Nyanda), Awadh Rashid (Alkadir), Joseph Lubasha (Villa Squad), Salvatory Nkulula (Red Star), Godson Naftal (Visanakabulu), Ismail Moshi (Orange Academy), Basil Seif (Kinondoni), Mustafa Rashid (Ruvuma), Thabit Kinyunyi (Ruvuma), Seleman Jumanne (Mara), Hassan Ally (Mara), Peter Manyika (Jitegemee), Mohamed Hassan (Mbande), Joseph Seleman (Jitegemee), Rajab Mwalimu (Kinyerezi), Bakari Ally (Twiga), Hassan Twiga (Twiga), Soud Shafi na Ahmed Merey.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 maoni:
Post a Comment