Tuesday, September 13, 2011

AJALI YA MELI ZANZIBAR



CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pole kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutokana na vifo vilivyotokea vya watu zaidi 200 baada ya kuzama kwa meli ya ya Mv Spice Islander mwishoni mwa wiki Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

TASWA inaungana na Watanzania katika kipindi hiki kigumu, huku tukiwaombea waliofariki Mwenyezi Mungu ahifadhi roho zao mahali pema peponi na wale majeruhi awape nguvu wapone haraka waweze kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.

Tunaziomba familia zilizopoteza ndugu zao ziwe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na waamini kwamba huo ni msiba wetu sote na si wao peke yao.

TASWA inaamini wapo wanamichezo waliopoteza maisha kwenye meli hiyo na pia wapo wanamichezo waliopoteza ndugu na jamaa zao, wote tunawapa pole na wawe na moyo wa subira.

(B)SEMINA YA WANAHABARI MOROGORO/ARUSHA.

Maandalizi kuhusiana na semina ya waandishi wa habari za michezo iliyopangwa kufanyika Septemba 25/25 mwaka huu mkoani Morogoro yanaendelea vizuri.
Sekretarieti ya TASWA itakutana Jumatano Septemba 14 jijini Dar es Salaam kuteua majina ya washiriki wa semina hiyo na ile itakayofanyika mkoani Arusha Oktoba 15/16 mwaka huu.

Tunaamini waandishi walio wengi watakuwepo kwenye semina hizo ama ya Morogoro au ya Arusha, isipokuwa wahariri wa habari za michezo ambao utaratibu unafanyika ili nao ifanyike ya kwao muda mfupi baada ya kumalizika semina ya Arusha.

Sekretarieti baada ya kuteua majina hayo itawasiliana na wahariri ambao waandishi wao wameteuliwa ili kupata maoni yao kwa vile uteuzi wa awali unaonesha baadhi ya vyombo wapo zaidi ya watatu, hali ambayo inaweza kuathiri utendaji wa chombo husika, lakini kama Mhariri akibariki uteuzi TASWA haitakuwa na tatizo.

Hivyo Alhamisi Septemba 15/2011, viongozi wa TASWA watafanya mkutano na wanahabari kwenye hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), saa tano kamili asubuhi kutangaza mdhamini wa semina ya Morogoro na majina 40 ya washiriki. Wote nawakaribisha.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU