Sunday, September 11, 2011

NBC YATOA MSAADA WA WAHANGA WA AJALI ZANZIBAR

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Haji Duni (katikati) akizungumza
baada ya kupokea msaada wa vyakula, dawa, maji na misaada mingine ya
kibinadamu iliyotolewa na Benki ya NBC kwa ajili ya wahanga wa ajali
ya Meli ya MV Spice Islander iliyotokea usiku wa Septemba 10 visiwani
humo. Katikati ni Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja
na nyuma ya Masanja ni Ofisa Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina.
Hafla ilifanyika Zanzibar juz
: Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja
(kushoto) akikabidhi sehemu ya misaada iliyotolewa na NBC kwa ajili ya
wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander kwa Waziri wa Afya wa
Zanzibar Juma Haji Duni  Mjini Zanzibar juzi. Kulia ni Meneja wa Tawi
la NBC Zanzibar, Rajab Maalim
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Zanzibar, Rajab Maalim (kulia)
akizungumza katika hafla ambayo NBC ilikabidhi  msaada wa vyakula,
dawa, maji na misaada mingine ya kibinadamu iliyotolewa na benki hiyo
kwa ajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander iliyotokea
usiku wa Septemba 10 visiwani humo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika
visiwani humo mwishoni mwa wiki. Katikati ni Waziri wa Afya wa
Zanzibar, Juma Haji Duni na wa pili kushoto ni Mshauri  wa Mambo ya
Habari wa NBC, Redemptus Masanja.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU