Thursday, September 29, 2011

MAFUZO YA WAANDISHI WA MICHEZO KUFUNGULIWA MOROGORO

MBUNGE wa Morogoro Mjini, Aziz Abood atafungua mafunzo ya waandishi wa habari za michezo yatakayofanyika kwa siku mbili Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.

Washiriki wataondoka Dar es Salaam Ijumaa Septemba 30, 2011, eneo la Ubungo Maji saa tisa alasiri, ambapo Mkuu wa Msafara atakuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Maulid Kitenge.

Viongozi wengine wa TASWA ambayo ndiyo imeandaa mafunzo hayo yakidhaminiwa na Vodacom na Kampuni ya mabasi ya Al Saedy watakuwa ni Mhazini Sultani Sikilo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Salum Jaba.

Mafunzo hayo yatakayoshirikisha waandishi 40 kutoka mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam yatafungwa Jumapili Oktoba 2, 2011 alasiri na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera.

Mafunzo yatakuwa katika sehemu mbili, ambayo ni taalum ya habari itakayofanyika Jumamosi na masuala yahusiyo sheria za michezo ya wavu na netiboli ambayo itafanyika Jumapili.

TASWA inawatakia kila la heri washiriki wote, huku ikiamini mafunzo hayo yatakuwa na manufaa makubwa kwao na kufanya vizuri kwao itakuwa ni fursa nzuri ya kuandaa mafunzo mengine kwa kadri itakavyowezekana.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU