Saturday, September 24, 2011

MARAIS WA KIAFRIKA WANAPOTANGAZWA WAMESHINDA MUDA HUO HUO BILA KUSUBIRI HATA SHEREHE RASMI YA KUMWAPISHA/KUMPONGEZA USHINDI WAKE HUKIMBILIA KUAPISHWA; HII INAMAANISHA NINI!

                                                           Rais mpya wa Zambia Mh. Michael Sata
Rais wa Kenya Mwai Kibaki.
Naomba wachambuzi wa mambo ya Siasa na wana Demokrasia na Diplomasia waweze kunisaidia hili, wengi wa viongozi wetu wa Kiafrika mara wanapotangazwa kuwa wameshinda katika chaguzi zao hukimbilia kuapishwa mapema.
Hii inaashiria nini! kutokujiamini? Hamu ya Madaraka? Kuwapenda sana wananchi wake? ni sehemu tu ya utaratibu wa kila mgombea ambaye ameshinda au ni shinikizo tu kutoka nje ya Taifa lake? Naomba wachambuzi wanisaidie hili.
Kwa upeo wangu mdogo naamini kama nchi ambayo ina Demokrasia ya ukweli na wananchi wake wameandaliwa vizuri kuidumisha hiyo demokrasia, sioni sababu ya kiongozi ambaye ameshinda kwa haki kukimbilia kuapishwa haraka.
KAPINGAZ Blog inasema, WANASIASA JENGENI UWEZO WA KUJIAMINI NA WAFUNDISHENI WANANCHI WENU DEMOKRASIA YA KWELI HATA UONGOZI WENU UTAKUWA WA HURU, HAKI NA USAWA

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU