Thursday, September 1, 2011

RAI YA MDAU WA SIASA


Napenda nitoe Rai yangu kwa wananchi wote wa Mataifa yote Duniani hasa Mataifa ya Bara la Afrika. Kumekua na tabia ya viongozi wetu ambao tumewapa dhamana ya kutuongoza iwe kwa Demokrasia namaanisha kwa kuwachagua au kwa njia za utawala wa kifalme au Kichifu na vile vile na wale ambao wanaingia kwa njia ya kuupindua uongozi mwingine ambao upo madarakani.

Pindi kunapotokea matatizo yoyote ya kiutawala wao, hasa kipindi ambacho kunatokea wapinzani wao; hawa viongozi wamekua mstari wa mbele kuwashawishi wananchi wao wanaowatawala waweze kuukana kwa hali, mali na Nguvu utawala mwingine unaoonekana unataka kuingia madarakani; iwe kwa Demokrasia, kwa nguvu ya kijeshi/usaliti/uasi au hata kwa nguvu ya Umma.

Kitendo kama hiki kinapelekea maelfu na malaki ya wananchi hao kufa kutokana na mapigano ambayo yanatokea kwa ajili ya Viongozi hao kugombania madaraka ya kuweza kutawala ie Nchi, Jimbo, Kijiji, na hata kata.

Tuna mifano michavhe ambayo tumeiona hivi karibuni, mfano taifa la Every Coast ni taifa ambalo lilikua limetulia sana na wananchi wake wakawa wanaishi maisha mazuri na huku kwa wale ambao ni Wakulima walikua wanaliendeleza zao lao la kilimo cha Pareto ambalo linaipatia fedha nyingi taifa hili, lakini cha kustaajabisha Taifa hili liliingia kwenye msuko suko mkubwa wa kisiasa na kupelekea wananchi wa nchi hii kuuwana maelfu kwa maelfu, kwa sababu tu mmoja amekataa kutoka madarakani hilo nadhani wengi wetu tumeliona na sasa tuna jingine hili tunalo mpaka hivi sasa linaendelea; Libya, wananchi wa Libya kwa zaidi ya miezi nane sasa wako katika msuko suko wa kisiasa kutokana na kikundi ambacho kinaitwa ni cha waasi ambacho kinataka kuchukua madarara ya taifa hili, tunajionea wenyewe sasa hivi wananchi wa Libya wanavyo taabika hawana maji hawana umeme huduma mahospitalini ni za tabu sana. Lakini haya yote yanaletwa na nani, kimsingi ni viongozi ambao wapo madarakani ndio wanayoyaleta yote haya, wameshindwa kusoma alama za nyakati.

Rai yangu hii inabeba ujumbe wa kwamba viongozi hawa wote ambao nimewatola mfano hapo juu walikua wanawahakikishia wananchi wao hasa wale wanaowasapoti wasirudi nyuma tutakufa wote kwenye ardhi hii tuliyozaliwa, wako wapi sasa, mbona hawajathubutu kukimbia na wale waliokua wanawatetea, wamewaacha wakitaabika na hali duni ya maisha waliyonayo ili hali wao viongozi wakiwa wamejisalimisha sehemu salama salmin na Familia zao. Naomba we mtanzania unaesoma Rai hii bofya hapa uusikie wimbo wa Bushoke Dunia Njia http://www.youtube.com/watch?v=aqFJ_Uccqmc 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU