Baadhi ya Viongozi wa Wizara na Serikali na wadau wa Sekta ya Afya nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin
Burudani ya Muziki kutoka kwa Mjomba Bendi katika kunogesha sherehe za kufungwa kwa maadhimisho hayoBaadhi ya Wafanyakazi wa Idara mbalimbali za Wizara ya Afya wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara hiyo. Mhe. Lucy Nkya.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Dkt. Lucy Nkya akitoa hotuba ya kufunga maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru na Utoaji Huduma za Afya Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia mafanikio yaliyofikiwa katika kutoa huduma ambazo hazikuwa zikipatikana hapa nchini kama vile Tiba ya Mfupa na Viungo, Upasuaji wa Moyo, Saratani na Tiba ya Magonjwa ya Figo pamoja na kusafisha Damu.
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya akielekea kukagua mabanda yaliyokuwa yanatoa huduma za Upimaji na Matibabu Bure kwa Wananchi wote.
Mgeni rasmi na Ujumbe wake wakipata maelekezo kutoka kwa Sada Nabos Nachundu wa Nzasa W. Group wanaotengeneza bidhaa mbalimbali za lishe kwa kutumia unga wa zao la Mtama.
Mganga Mtafiti wa Tiba Asilia na Magonjywa Sugu na Ukimwi Tanzania kutoka M.M.D.K Dkt. Ahmadi Darusi Salim akitoa maelezo kwa Mhe. Mgeni Rasmi ya Dawa inayotumiwa na Wagonjwa waliothirika na Virusi vya Ukimwi kwa ajili ya kuimarisha Afya zao. Ambapo mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya alimshauri kupeleka dawa wanazozitafiti katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ili kuhakikiwa.
0 maoni:
Post a Comment