Tuesday, October 11, 2011

MASHINDANO YA MITUMBWI YA BALIMI EXTRA LAGER 2011 YAZINDULIWA RASMI.

Mashindano hayo ya kupiga kasia, yanayo dhaminiwa na bia ya “Balimi Extra Lager”  yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera na visiwa vya Ukerewe. Mashindano haya yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Edith Bebwa alisema, Ni zaidi ya miaka sita sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, kwa kipindi chote hiki tumefanikiwa kuleta changamoto katika upigaji makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika. Mashindano haya ya mitumbwi ya Balimi sasa yamekuwa na umaarufu mkubwa na kuongoza kwa mashabiki katika kanda ya ziwa.  

Kama ilivyo kawaida, mashindano haya yatatanguliwa na burudani mbalimbali za uhamasishaji, zikifuatiwa na mpambano katika hatua ya mwanzo kabla ya fainali kuu itakayofanyikia Jijini Mwanza tarehe 18 Desemba. Katika hatua za awali mashindano yataanzia Kituo cha Mwanza tarehe 23 Oktoba, Kigoma na Kagera tarehe 5 Novemba, Mara na Ukerewe tarehe 19 Novemba. Pia ninapenda kuwajulisha washiriki kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa zaidi, ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hivyo washiriki waongeze mazoezi ili kujihakikishia ushindi katika maeneo yao, pia timu tatu za wanaume na mbili za wanawake zitakazoshika nafasi za juu zaidi katika ngazi ya awali ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza.

Zaidi wataochukuwa ubingwa mwaka huu upande wa wanaume na wanawake watapata  fursa ya moja kwa moja ya kuingia finali za mwaka ujao ili kutetea ubingwa wao.

Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za awali na fainali, Meneja Masoko wa Tbl Bwana Fimbo Butallah alisema; Katika ngazi za mikoa zawadi zitakuwa kama ifuatavyo:


Ngazi ya Mikoa

Fainali Kuu

Wanaume
Wanawake

Wanaume
Wanawake
Mshindi wa kwanza
                800,000
                 600,000

              2,600,000
                 2,200,000
Mshindi wa Pili
                600,000
                 500,000

              2,200,000
                 1,600,000
Mshindi wa Tatu
                400,000
                 300,000

              1,600,000
                    850,000
Mashindi wa Nne
                350,000
                 250,000

                  850,000
                    600,000
5 hadi 10 - Kila timu
                200,000
                 150,000

                  400,000
                    200,000

Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu ya ushindani kwa washiriki na hivyo kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki. Tunawaomba wakazi wa kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano haya ya aina yake.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU