Friday, October 14, 2011

MTANZANIA AOMBEWA ITC UJERUMANI

MCHEZAJI Costancia Maringa wa Tanzania ameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili aweze kucheza mpira wa miguu wa wanawake nchini Ujerumani.
 
Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB) kimetuma maombi hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya FC 1919 Marnheim ya nchini humo.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa DFB, Helmut Sandrock, Maringa mwenye umri wa miaka 12 ameombewa ITC na chama hicho kama mchezaji wa ridhaa. TFF inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika kukamilika.
 
LIGI DARAJA LA KWANZA
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza hatua ya makundi msimu huu inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaanza Oktoba 15 mwaka huu. Jumla ya timu 18 zinashiriki katika ligi hiyo.
 
Kundi A kesho itakuwa Temeke United vs Polisi Dar es Salaam (Uwanja wa Mlandizi, Pwani) na Mgambo Shooting vs Transit Camp (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga). Mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Burkina na Morani itachezwa Oktoba 16 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.  
 
Mechi za kundi B kesho ni Polisi Iringa vs Small Kids (Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora, Iringa), Tanzania Prisons vs Mbeya City (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya) na Mlale JKT vs Majimaji (Uwanja wa Majimaji, Songea).
 
Kundi C kesho ni AFC vs Manyoni (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Polisi Morogoro vs 94 KJ (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Polisi Tabora vs Rhino (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
 
Ligi hiyo itaendelea tena Oktoba 19 mwaka huu kwenye viwanja tofauti. Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 30 mwaka huu na kupisha dirisha dogo la usajili litakaloanza Novemba 1 hadi 30 mwaka huu. Mzunguko wa pili wa ligi hiyo utaanza Januari mwakani.
 
VIINGILIO SIMBA VS AFRICAN LYON
Viingilio katika mechi namba 62 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na African Lyon itakayochezwa Oktoba 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam vitakuwa kama ifuatavyo;
 
VIP A itakuwa sh. 15,000, VIP B sh. 10,000, VIP C sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa (orange straight and curve) sh. 5,000 wakati viti vya kijani na bluu itakuwa sh. 3,000.
 
Mechi hiyo itaanza saa 10 jioni na tiketi zitauzwa uwanjani kwenye magari maalumu.
 
LIGI KUU YA VODACOM
Mechi za wiki hii za Ligi Kuu ya Vodacom ni kama ifuatavyo;
Oktoba 15- JKT Ruvu vs Azam (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 16- Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa)
Oktoba 19- Simba vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 20- Yanga vs Toto Africans (Uwanja wa Taifa)
Oktoba 21- Azam vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 22- Simba vs JKT Ruvu (Uwanja wa Taifa)
Oktoba 23- Yanga vs Oljoro (Uwanja wa Chamazi)
 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU