Sunday, October 23, 2011

NBC YAANDAA TAFRIJA KWA WADAU NA WANACHAMA WA PPF

 Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni wa NBC, Bi. Minnie Kibuta
(kushoto) akimsevu chakula Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa
Mashirika ya Umma (PPF) William Erio katika hafla iliyoandaliwa na NBC
kwa wadau na wanachama wa PPF waliokuwa katika mkutano wao mjini
Arusha mwishoni mwa wiki
: Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni wa NBC, Bi. Minnie Kibuta
akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na NBC
kwa wadau wa PPF mjini Arusha mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma William
Erio (katikati) akishikana mikono na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa
Benki ya NBC, Mwinda Kiula-Mfugale wakati wa hafla ya chakula cha
jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa wanachama na wadau  waliokuwa
wakihudhuria Mkutano Mkuu wa 21 wa  PPF  jijini Arusha mwishoni mwa
wiki. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni, Minnie Kibuta.
Baadhi ya wadau wa PPF wakifurahia vinywaji katika hafla hiyo
pembeni ya jiko la moto lililowekwa kwa ajili ya hali ya hewa ya
kibaridi iliyopo mjini Arusha kwa sasa
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF)
William Erio (kulia) akishikana mikono na Meneja Mahusiano wa Benki ya
NBC, Bi. Robi Matiko-Simba wakati wa hafla ya chakula cha jioni
kilichoandaliwa na benki hiyo kwa wanachama na wadau  waliokuwa
wakihudhuria Mkutano Mkuu wa 21 wa  PPF  jijini Arusha mwishoni mwa
wiki. Katikati ni Meneja Mahusiano wa PPF, Bi. Lulu Meleng
                                      Kikundi cha wamasai kikitoa burudani katika hafla hiyo.
Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto)
Ofisa Uhusiano, Eddie Mhina na mdau wa PPF Muhidini Michuzi wa Globu
ya Jamii wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo mjini Arusha
mwishoni mwa wik

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU