Klabu ya Yanga imemuangukia aliyekuwa mfadhili wake Yusuph Manji, wakimtaka alejee kuisaidia timu hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga, alisema kwamba Klabu yao imekuwa na matatizo ya kufungwa mechi mbili na kutoka sare baadhi ya mechi, hivyo kuwa kwenye nafasi ya tano kitu ambacho siyo kawaida yao.
NCHUNGA amesema wamekuwa na mazungumzo na majadiliano ya muda mrefu na mfadhili zamani yusuph Manji, ambaye alijitoa katika kuifandhili klabu na kubaki kama mwanachama wa kawaida mtiifu
Alisema hiyo ilitokana na ukweli kwamba pengo lake limekuwa ni dhahiri katika kuendeleza Yanga na kipindi chote alichoondoka hakuna mfadhiri wa aina yake aliyewahi kujitokeza japo wakorofi wachache walimbeza.
Nchunga alisema Ingwa wana mikakati endelevu ya kujitegemea kama vile kuuza vifaa vyenye Logo yao ambapo wameingi mkataba na kampuni ya NsajjereSports Wear na ujenzi wa Uwanja wa Kaunda utakaotupatia viingilio, pia na jengo la Mafia kama kitega uchumi , na uongezeko la wanachama kama rasilimali yao.
Alisema kwa mantiki hiyo, kuna mambo yaliyohitajika mkono wake kukamilika, nayo ni, ukarabati wa uwanja Kaunda, ujenzi wa jingo la Mafia na masuala mengine ya kimfumo ambayo mengi yako katika muafaka.
Alisema wamemuandikia barua manji kumuarifu hilo naye ameahidi kuwajibu pindi atakaporejea safariAliwaomba wanachama na wapenzi wa Yanga kumpokea kwa moyo mfadhili huyo na kumpokea kwa mikono miwili.Alisema kwa wale ambao watapenda kumpokea pale uwanja wa ndege siku kesho wanaweza kufanya hivyo.
0 maoni:
Post a Comment