Kocha Mkuu wa timu za Taifa za vijana, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya Taifa kwa vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kitakachoshiriki michuano ya umri huo ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano hiyo itafanyika Gaborone, Botswana kuanzia Desemba 1-10 mwaka huu ikishirikisha timu za mataifa 11 wanachama wa COSAFA na Tanzania inayoshiriki kama mwalikwa.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni Saleh Malande (Simba), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Suagr), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Said Samir (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Domayo (JKT Ruvu Stars) na Omega Seme (Yanga0.
Wengine ni Atupele Green (Yanga), Jerome Reuben (Moro United), Simon Happygod (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Abdallah Hussein (AFC), Rajab Mohamed (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Emily Josiah (TSC Mwanza), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting Stars).
Ngorongoro Heroes ambayo iko kundi D pamoja na Zambia, Afrika Kusini na Mauritius inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 30 mwaka huu kwenda Gaborone.
TENGA KUFUNGA KOZI YA CAF
Rais wa TFF, Leodegar Tenga kesho atafunga kozi ya ukocha kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyofanyika kuanzia Novemba 7 mwaka huu.
Ufungaji wa kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 30 utafanyika kuanzia saa 4.30 asubuhi katika ofisi za TFF. Kozi hiyo iliendeshwa na wakufunzi wanne, mmoja wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), wawili wa CAF na mmoja wa Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU).
Mkufunzi wa FIFA alikuwa Jan Poulsen, kutoka CAF ni Sunday Kayuni (Tanzania), Kasimawo Laloko (Nigeria) wakati kutoka Denmark ni Kim Poulsen.
Makocha walioshiriki ni Christopher Eliakim, Jumanne Ntambi, Keneth Mkapa, Mussa Furutuni, Mecky Maxime, Gideon Kolongo, Maka Mwalwisi, Haji Amir, Tiba Mlesa, Stephen Matata, Wane Mkisi, Leonard Jima na Ahmed Mumba.
Wengine ni Peter Mhina, Absolom Mwakyonde, Maarufu Yassin, Mussa Kamtande, Wilfred Kidau, Eliasa Thabit, Dismas Haonga, Fulgence Novatus, Juma Mgunda, Hassan Banyai, Mohamed Tajdin, Sebastian Nkoma, Emmanuel Massawe, Gabriel Gunda, Abdul Nyumba na Richard Kabudi.
0 maoni:
Post a Comment