Sunday, November 13, 2011

MBUNGE MO ATUMIA NUSU BILIONI, MIRADI YA MAJI JIMBONI MWAKE MWAKA HUU


MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini (CCM) Mohammed Ghulam Dewji ametumia zaidi ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji safi na salama vijijni katika kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Rc Mision Dewji maarufu kwa jina la MO alisema mradi huo utanufaisha jumla ya vijiji 10 vinavyozunguka jimbo hilo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake wakati wa uchaguzi Mkuu.
Alisema mara baada ya kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa Jimbo hilo  mwaka 2010, alianza kazi ya kuchimba visima katika vijiji hivyo ambapo alianza na visima saba na kunedela taratibu taratibu hadi kufikia visima 17.
Alisema visima hivyo vimetumia zaidi ya shilingi nusu bilioni hadi kukamilika kwake ambapo kati ya hivyo visima saba vinazinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi na yeye mwenyewe katika ziara ya siku nne jimboni humo.
“Hivi sasa visima saba tayari vinekamilika kwa aslimia 100 na vinatoa maji, lakini hivi kumi tayari vimeanza kuchimbwa na muda si mrefu navyo vitakamilika na kufanya jimbo lote sasa kupata maji safi na salama.” Alisema MO.
Aidha Mbunge huyo kijana alivitaja vijiji 10 ambavyo vinanufaika na mradi huo wa maji kuwa ni Mtipa, Manga, Ititi, Unyianga, Mtamaa A& B, Mwankoko A& B, Uhamaka na Kisaki.
“Unajua kilichonifanya mimi kugombea ubunge mwaka 2000 ni kutokana na kuona kuwa wananchi wa jimbo la singida mjini wana matatizo makubwa sana ya maji , na utakumbuka aliyekuwa Mbunge wa Jimbo  hili Mussa Nkangaa alikuwa waziri wa maji, kwa hiyo baada ya kupata ubunge jambo la kwanza nilianza na maji kwa hiyo hadi kufikia mwaka 2012- 2014 wananchi wangu hawatakuwa na tatizo la maji tena .”Alisisitiza MO.
Aidha alisema kutokana na jitihada hizo, kwa kuunganisha nguvu na mradi mkubwa wa maji katika mji wa singida unaofadhiliwa na  benki ya dunia (BADEA) na serikali ya Tanzania ya kubadilisha miundombinu yote ya maji katika mji huo.
Hata hivyo alisema dira yake ni kuihakikisha kuwa ifikapo 2014 jimbo zima vijiji vyote viitakuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa aslimia 100 na hivyo kuondoa dhana ya kina mama kuacha kufanya shughuli zingine za maendelea kwa kufuata maji umbali mrefu

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU