Monday, November 14, 2011

ZIARA YA MO KATIKA MRADI WA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA UNAOFADHILIWA NA BADEA SINGIDA MJINI.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na taka Singida, SUWASA, Marin Churi akifafanua jambo kwa ugeni ulioambatana na Mbunge wa Singida Mjini,Mohammed Dewji (kushoto) kwenye msafara huo wakiwemo viongozi wa siasa.
Mbunge wa Singida Mjini Mohammed Dewji akihoji juu ya mambo ya mradi wa maji mkubwa wa maji uliofadhiliwa kwa msaada wa BADEA, kwa viongozi wa juu wa SUWASA:Mkurugenzi wa SUWASA,Injinia Isaack Nyalonji Akitoa maelezo ya kisima kikubwa cha mradi wa BADEA katika eneo la Mwankoko, kushoto kwake Mbunge Mo Dewji alipotembelea kukagua mradi huo ambao unatarajia kumalizika Julai mwakani. Wa pili kushoto, Mstahiki Meya, Shehe Salum Mahami, eneo la chanzo cha mradi huo wa maji
:Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji akisalimiana na watendaji wakuu wanaosimamia mradi huo wa BADEA, Mr. Ragpathy (Contracts Manager) pembeni yake, Ashork Patel (Site Incharge) wa kampuni ya SPENCON SERVICE LTD
Dewji akipata maelezo ya sehemu mbalimbali ndani ya eneo la Ujenzi la mradi wa Tanki kubwa na la kisasa kutoka kwa mmoja wa wataalum wa kampuni ya Spencon Service Ltd alipotembelea huko eneo laMo Dewji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa mradi huo wa BADEA ambao unatarajiwa kumalizika Julai mwakani
Mo Dewji akihoji swali juu kwa wataalum wanaoshughulikia mradi huo wa usambazaji maji mjini, maarufu kama BADEA, alipotembelea katika eneo hilo
Moja ya Tanki la maji ambalo litakua likipokea maji na kusambaza sehemu nyingine mbalimbali. Mradi huu unajengwa na wataalamu kutoka kampuni ya Spencon Service Ltd
Tanki la maji likiwa kwenye hatua ya ujenzi linavyoonekana kwa sasa ambapo ujenzi wake unatarajia kumalizika mwakani, ambapo mradi huo utakuwa na matumaini makubwa kwa wananchi wa Singida ukikamilika .

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU