Tuesday, December 13, 2011

MECHI ZA CHALENJI ZAINGIZA MIL 267


Mechi 26 za michuano ya 35 ya CECAFA Tusker Challenge Cup iliyofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 mwaka huu zimeingiza sh. 267,066,000. Michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ilishirikisha timu za mataifa 12.
 
Hatua ya makundi ya michuano hiyo iliingiza sh. 145,613,000, robo fainali (sh. 58,470,000), nusu fainali (sh. 55,787,000) wakati fainali iliingiza sh. 17,196,000. Kila siku zilichezwa mechi mbili isipokuwa Novemba 26 mwaka huu ambapo ilikuwa siku rasmi ya ufunguzi na Novemba 28 mwaka huu zilichezwa mechi tatu.
 
Mechi iliyoingiza fedha nyingi kuliko zote ilikuwa ya ufunguzi hatua ya makundi kati ya Tanzania na Rwanda ambapo zilipatikana sh. 64,178,000 wakati fedha kidogo (sh. 446,000) zilipatikana kwenye mechi kati ya Uganda na Somalia iliyochezwa Novemba 28 mwaka huu Uwanja wa Azam.
 
Jumla ya washabiki walioshuhudia michuano hiyo walikuwa 103,312. Washabiki walioshuhudia hatua ya makundi walikuwa 65,617, robo fainali (17,844), nusu fainali (16,014) wakati fainali walikuwa 4,837.
 
Mechi iliyokuwa na washabiki wengi zaidi ni kati ya Tanzania na Rwanda ambapo waliingia 23,946 wakati iliyoingiza wachache ni 446 walioshuhudia mechi kati ya Somalia na Uganda.
 
Tunawashukuru wadhamini wakuu Tusker na washabiki waliojitokeza kushuhudia michuano hiyo. Vilevile Kampuni ya mafuta ya Gapco, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na PSPF, na pia wadau wengine waliofanikisha mashindano hayo kwa njia mbalimbali akiwemo Zacharia Hanspope.
 
37 KUSHIRIKI SEMINA YA GRASSROOTS
 
Washiriki 37 wameteuliwa kushiriki katika semina ya grassroots inayolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 kutoka Mkoa wa Dar es Salaam itakayofanyika kuanzia Desemba 14-17 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
 
Mbali ya walimu wa shule za msingi ambao ndiyo wengi, washiriki wengine wanatoka Kamati za TFF za Mpira wa Miguu ya Vijana na Mpira wa Miguu wa Wanawake. Semina hiyo itakayokuwa chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gouinden Thondoo kutoka Mauritius ambaye ameshawasili nchini itamalizika Desemba 17 mwaka huu kwa tamasha (festival) litakalofanyika Uwanja wa Taifa na kushirikisha watoto 1,200.
 
Washiriki wa semina hiyo ni Maria Tarimo, Magreth Mainde, Isaac Muhanza, Lucian Boniface, Hassan Msonzo, Hadija Kambi, Charles Kiwero, Abdul Mwarami, Florence Ambonisye, Sophia Willbest, Muhidin Manish, Rajab Asserd, Rebecca Joseph, Mussa Kapama, Rukia Mkai, Phoebe Lugana na Imani Mwalupetelo.
 
Idd Luena, Dina Muhomba, Ally Chanda, David Kivinge, Juma Ally, Seif Koja, Raymond Gweba, Farij Bukuji, Gema Matagi, Joyce Sanka, Stella Seng’ongo, Hassan Seleman, Ramadhan Yahya, Maua Rashid, Paul Chagonja, Ali Mtumwa, Daud Yassin, Michael Bundala, Raphael Matola na Furaha Francis.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU