Tuesday, December 13, 2011

RAIS ATEMBELEA MAONYESHO YA UHURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Mratibu wa Maafa katika  Idara ya Uratibu wa Maafa , Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Gilbert Mkindi , alipotembelea banda hilo katika  Maadhimisho  ya Kitaifa ya Miaka 50 ya  Uhuru  wa Tanzania Bara katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere,  Jijini Dar es Salaam  tarehe 11 Desemba, 2011,   Kushoto ni Mkurugenzi msaidizi (Oparesheni) Bibi. Nyancheghe Nanai, na kulia ni Mratibu Maafa Bw. Fanuel Karugendo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Afisa Uwekezaji wa  Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Brandon Maro  alipotembelea banda hilo katika  Maadhimisho  ya Kitaifa ya Miaka 50 ya  Uhuru  wa Tanzania Bara katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere,  Jijini Dar es Salaam  tarehe 11 Desemba, 2011,   Kushoto ni Mkurugenzi (Utafiti, Sera na Mipango) Bw. Joel Kyaruzi.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU