Wednesday, January 18, 2012

AIRTEL YATOA MSAADA WA KOMPYUTA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI ARUMERU ARUSHA

 Ofisa Uhusiano wa kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel,Jane Matinde akikambidhi  sehemu ya msaada wa kompyuta  4,Mbunge wa Arumeru Magharibi na Naibu waziri wa Ardhi ,nyumba maendeleo na makazi Bw. Goodluck Ole Medeye  kwa ajili ya shule  ya sekondari  ya Mlangarini iliyoko Wilayani  Arumeru Mkoani Arusha.
 Ofisa Uhusiano wa kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel,Jane Matinde akimuelekeza jambo Mbunge wa Arumeru Magharibi na Naibu waziri wa Ardhi ,nyumba maendeleo na makazi Bw. Goodluck Ole Medeye  baada ya kumkabidhi kompyuta  4 kwa ajili ya shule ya ya sekondari  ya Mlangarini iliyoko Wilayani  Arumeru Mkoani Arusha,na kushoto ni Diwani wa kata ya Mlangarini,
Bw.Mathias Erasto akishuhudia tukio hilo.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari  ya Mlangarini iliyoko Wilayani  Arumeru Mkoani Arusha,Bw. Elisa John Pallangyo akitoa maneno ya shukurani kwa kampuni ya simu ya Airtel kwa msaada mkubwa walioutoa kwa ajili ya shule hiyo,pichani kati ni mgeni rasmi wa tukio hilo adhimu Mbunge wa Arumeru Magharibi na Naibu waziri wa Ardhi ,nyumba maendeleo na makazi Bw. Goodluck Ole Medeye ,sambamba na Diwani wa kata ya Mlangarini,Bw.Mathias Erasto akishuhudia tukio hilo na shoto ni Ofisa Uhusiano wa Airtel.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa computer 4 kwa shule
ya sekondari Mlangarini iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha  ikiwa
ni moja wapo kati ya shughuli za kutoa huduma zinazofanya na kampuni
hiyo kwa jamii huku lengo hasa likiwa ni kukuza sekta ya elimu nchini

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel, Afisa
uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema, Airtel inajisikia faraja
kutembelea shule ya Mlagarini na kuwapatia computer zitakazowawezesha
kupata  vitabu mbalimbali kwa njia ya mtandao na kutoa fulsa kwa
wanafunzi  wa sekondari kujifunza kutumia computer wakiwa bado
mashuleni. Aidha aliahidi kuwa Airtel  itaendelea kushiriikiana na
serikali  kupitia wizara ya elimu katika kuhakikisha elimu mashuleni
inaboreshwa.

Akiongea baada ya kukabidhiwa computer hizo Mbunge wa Arumeru
Magharibi na Naibu waziri wa Ardhi Nyuma Maendeleo na Makazi Bw.
Goodluck Ole Medeye alisema. Tunashukuru sana kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel kwa kuipatia shule ya sekondari Mlangarini computer
zitakazowawezesha kupata habari na vitabu mbalimbali kwa njia ya
mtandao, computer hizi zitarahisisha sana upatikanaji wa nyezo muhimu
za elimu kwa wanafunzi na walimu kwa kupitia mtandao.

Pia aliwaasa wanafunzi wa  mlangarini kutumia fulsa hiyo kujifunza na
si kutumia computer hizo kuangalia mambo yasiyofaa katika internet Ole
madeye aliendelea kuwaasa na kuwapa changamoto  wanafunzi  kuweza
kupana akili za na kuwa wavumbuzi wa vifaa muhimu zitakavyosaidia
jamii kama ilivyovumbuliwa computer hiyo.

Pamoja na haya alifafanua kuwa computer hizo zitatumika pia kwa wakazi
wa maeneo hayo kwani makitaba ya wilaya itakuwa hapa shuleni hivyo
basi wakazi wa wilaya ya Arumeru watapata fulsa ya kutangaza biashara
zao kwa kupitia mtandao na kuweza kupata taarifa muhimu zitakazo
wasaidia katika kuboresha biashara zao na shughuli muhimu za wilayani
hapo pia aliongeza Madeye.

Naye Diwani wa kata ya Arumeru Bw Martias Manga alichukua fulsa pia
kuwashukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kuwaasa wanafunzi
kutumia computer hizo vizuri na kuzitunza ili zisaidie wanafunzi wengi
zaidi shule hapo. Aliwaasa wanafunzi hao kuchukua nafasi hii ya pekee
kujifunza na kutumia computer hizo katika kujijenga kielimu na
kitaaluma zaidi

Akitoa shukurani Mwalimu mkuu wa shule Elisa John Pallangyo
ameipongeza Airtel kwa kuwafikishia msaada muhimu shuleni hapo na
kuahidi kwa kupitia msaada kiwango cha elimu shuleni hapa kitapanda
kwani changamoto mbalimbali walizokuwa nazo kama vile internet,
upatikanaji wa nyenzo muhimu katika kufundishia  zitapungua kwa kiasi
kikubwa sana.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
kama vile Vitabu vya shule ya sekondari,  kuchangia katika huduma za
afya ambapo wiki iliyoopita waligawa baskeli kumi katika vituo vya
afya wilayani misungwi na kutoa mchango wao pia katika sekta ya
michezo kwa kudhamini michezo mbalimbali nchini.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU