Saturday, January 28, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMALIZIA ZIARA YA MKOA WA TANGA, WILAYANI LUSHOTO

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto baada ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo hilo lililopo Chakechake Lushoto jana Januari 27, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Sophia Mjema.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasalimia na kuwaaga wasanii waliokuwa wakitoa burudani, wakati akiondoka Chakechake baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, jana Januari 27, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa mbogamboga, Juma Kambaga, kuhusu uzalishwaji wa mbogamboga hizo wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia chupa ya Juisi iliyotengenezwa na wajasiliamali, Salome Mtawa (kulia) wa kikundi cha Usambara Lishe Trust,  wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkulima wa Nyanya, Judith Munis, wa Kikundi cha Upendo Jegestal, kuhusu kilimo cha nyanya, wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga.


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU