Saturday, February 18, 2012

HATIMAE YANGA NA ZAMALEK ZATOKA SARE

Mashabiki Lukuki wa timu ya Yanga wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ajili ya kuipa sapoti timu yao inayojitupa uwanjani muda si mrefu kumenyana na timu ya Zamaleck ya Misri kwenye mashindano ya klabu Bingwa Afrika.hivyo Libeneke la Globu ya Jamii leo litakuwa bega kwa bega wa Wadau wote kuhakikisha mnapata kina kinachojiri uwanjani hapa.
Hatati langoni mwa timu ya Zamaleck.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Khamis Kiiza akishangilia goli lake la kwanza alilolipachika dakika ya 36 na katika kipindi cha pili Zamalek wakajipatia bao.

Bao la Amri Zakhi wa Zamaleki ya Misri, kunako dakika ya 74 ya mchezo, limeiweka klabu ya soka ya Yanga ya Tanzania katika wakati mgumu wa kufuzu hatua ijayo ya michuano ya Kombe la Washindi Barani Afrika, baada ya kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya wakali hao toka Afrika ya Magharibi.


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU