Monday, February 20, 2012

MASHINDANO YA GOLFU YA GOLF ROTARY DAY 2012

Mashindano ya golfu ya  Golf Rotary day 2012 yaliyofanyika katika viwanja vya gymkana Arusha yamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 120 kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa maji safi kwa familia 500 zisizojiweza zikiwemo hospitali na mashule.

Mshindi wa jumla katika Mashindano hayo ya mwaka 2012 ambayo yaliandaliwa na Arusha rotary club ni  Richard Gomes aliyepata point 39 akifuatiwa na mwenyekiti wa golfu tanzania Paul Mathison aliyekuwa mshindi wa pili na kupata point 38 na kwa upande wa wanawake mshindi wa jumla alikuwa Neema Olomu aliyepata point 38.

Mashindano hayo yalidhaminiwa na kampuni ya uuzaji magari ya Hughes Motors ya jijini Arusha na kushirikisha wachezaji zaidi 81 kutoka Kenya,TPC MOSHI, TIMU YA GOLFU YA TANZANITE ONE na wachezaji mbalimbali wa golf wa mjini humo.

Kaimu meneja mkuu wa Kampuni ya Hughes motors Robert  Odundo amesema lengo la kudhamini mashindano hayo ni kurudisha fadhila kwa wateja wao kwa kusaidia jamii zisizojiweza ili ziweze kupata maji safi na salama na kuahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo kila mwaka.

Insert Robert …………………………..

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa rotary club ya Arusha Zina DALLE amewashukuru wale wote waliojitokeza kucheza kwa ajili ya kuchangia huduma hiyo kwa ajili ya kusaisaidia jamii kupata maji safi ya uhakika katika maeneo wanyoishi.

Insert……………… Zina DALLE mwenyekiti kamati ya maandalizi wa rotary club ya Arusha

Inserts wachezaji  Paul Mathison mchezaji back to back



0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU