kushoto ni mmiliki wa Orion Tabora hotel na mdhamini wa mashindano ya Tabora Marathon 2012,na kulia ni mratibu wa mashindano hayo Ramadhan Makula
.
CHAMA cha riadha mkoa wa Tabora,(RITAM),kwa kushirikiana na Orion Tabora Hotel,wanatarajia kuendesha mashindano yatakayojulikana kama Tabora Marathon 2012 kwa lengo la kuutangaza mkoa na vivutio vyake.
Mratibu wa mashindano hayo,Ramadhan Makula,akizungumza na waandishi wa habari,katika Orion Hotel,alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji,kutangaza vivutio vilivyoko Tabora na kuaandaa vijana katika medani ya kitaifa na kimataifa.
Makula alisema wadhamni wa mashindano hayo ni Orion Tabora Hotel,chini ya usimamizi wa mkurugenzi wa hotel hiyo Poley Ahmed na mashindano hayo yanatarajia kushirikisha watu 400 wa rika mbalimbali.
Aliongeza maeneo hayo yataboreshwa kwa kupaka rangi hali ambayo itawawezesha wananchi na wageni mbalimbali kupata fursa ya kutembelea maeneo hayo ambayo yako kwenye historia ya nchi.
Maratibu huyo alisema wmeamua kufanya hivyo kwa kuwa wana uzalendo mkubwa na mkoa wa Tabora kwani bado mkoa haupewi kipaumbele licha ya kuwa ni mkoa wenye uiwingi wa mambo ya utalii na hata kisiasa.
0 maoni:
Post a Comment