Friday, February 17, 2012

TAARIFA KUTOKA (TPBC)

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) imeanza mazungumzo ya awali ya kuingia kwenye mkataba wa miaka mitano na Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Kikao cha kwanza cha makubaliano haya kilifanyika tarehe February 16, 2012 jijini Arusha ambapo suala zima la Utalii wa Michezo (Sports Tourism) lilitawala.

Katika mazungumzo hayo, Jiji la Arusha liliwakilishwa na Mstahiki Meya Gaudence Lyimo na Naibu Meya Sakeyan. Kwa upande wa TPBC, IBF na CBC waliwakilishwa na Rais wake Onesmo Ngowi pamoja na Kamishna wa TPBC mkoa Arusha Roman Chuwa ambaye ni mfanyabishara wa utalii anayemiliki kampuni ya Equatorial Safaris and Tours ya jijini Arusha

Makubaliano haya ambayo yanarajia kuzaa mkataba wa miaka mitano kati ya wabia hawa (Halmashauri ya Jiji la Arusha na TPBC) yanalenga kujenga ajira kwa vijana, kutangaza jiji la Arusha kama kitovu cha utalii wa ndani na nje (Destination Market), kujenga biashara za nje (Foreign trades) pamoja na kuanzisha na kuendeleza mtandao vituo (Sports gyms) vya mafunzo ya kuibua vipaji vya michezo kwa vijana katika kata zote za Jiji la Arusha.

Katika makubaliano haya, Ngowi anawakilisha pia Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) lililo na makao makuu yake makuu jijini New Jersey, nchini Marekani ambalo litatumika kutangaza jiji la Arusha kama kitovu cha biashara ya kitalii kwa wananchi wa Marekani na nchi zote za Amerika ya Kaskazini, Kusini ya Caribbean.

IBF ina mtandao katika nchi zaidi ya 78 na itasaidia sana kutangaza jiji la Arusha kwenye mtanado wake.

Mkataba huo pia unajumuisha Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola Commonwealth Boxing Council (CBC) ambalo Onesmo Ngowi ni Mkurugenzi wa Bodi yake. CBC litatoa vibali vya mapambano ya kugombea ubingwa wa Jumuiya ya Madola.

Aidha, makubaliano haya yatalipatia jiji la Arusha mapambano manne (4) ya kimataifa kwa mwaka yatayosimamiwa na IBF ambayo yatarushwa na luninga kwenye nchi zaidi ya 78 duniani zikiweko Marekani, nchi za Ulaya, Japan na Australia ambazo ndio chemecheem kubwa ay watalii Tanzania.

Imetolewa na

Onesmo A.M.Ngowi

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU