Tuesday, March 20, 2012

AFYA YA KAMANDA GULUMO INAENDELEA VIZURI

 
Msanii Mkongwe wa bendi Kwongwe ya Msondo Ngoma Music,Muhidini Gurumo  akiwa katika hospital ya Taifa Muhimbili, Dar es salaam jana, akipimwa  mapigo ya Moyo na Ofisa Muuguzi Msaidizi wa Hospital hiyo,Suraiya  Mohamed alipolazwa kufanyiwa uchunguzi wa kina toka mwishoni mwa wiki iliyopita.

MWANAMUZIKI maarufu wa bendi kongwe ya  Msondo ngoma, Muhidin Gurum  aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugojwa wa shinikizo la damu anaendelea vizuri.


Akizungumza na Dar es Salaam jana,Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila
'Super 'D' alisema Afya ya  Gurumo inaendelea vizuri na wakati wowote
anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Alisema kuwa madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kwa kina
kujua kila kitu kinachop msumbua  katika mwili wake.

"Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofauti  na mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza hakurusiwa hivi karibuni.

Hata hivyo aliwataka wapenzi wa bendi hiyo kumuombea duwa mwanamziki huyo ili apone upesi pia aliongeza kwa kusema maonesho yao ya wiki hii ni kama ifuatavyo Alhamisi watakuwa Mwandege Mkoa wa Pwani,Ijumaa
watapiga katika viwanja vya Lidaz Clab jumamosi watakuwa katika viwanja vya TCC Sigara na Jumapili watamaliza wiki endi katika ukumbi wa Max Bar uliopo Ilala Bungoni

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU