Monday, March 12, 2012

AIRTEL TANZANIA YAZINDUA PROGRAMU YA KUWAWEZESHA WASICHANA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI.

wanafunzi wa shule ya  sekondari  Canossa   iliyopo Tegeta jijini Dar-es-salaamani wakionyesha ushirikiano kwa kunyoosha mkono ikiwa ni moja ya utaratibu uliotumika ili kuchaguliwa kujibu swali wakati wa mada maalum iliyotolewa na Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja bi Adriana Lyamba wakati wa semina maalum kwa wanafunzi hao yenye  lengo la kuwawezesha wasichana kujiamini na kuwa na mbinu za kufikia malengo yao.
Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Bi.Tunu Kavishe(kushoto aliesimama) akimwelekeza mmoja wa  wanafunzi wa shule ya  sekondari  Canossa  iliyopo Tegeta jijini Dar-es-salaam wakati wa uzinduzi wa programu  mpya   ya kuwawezesha wasichana wa shule za sekondari  kuweza kujiamini na kufanya maamuzi sahihi yatakayowafaa katika  kutimiza malengo yao ya baadae na  jinsi ya kufikia malengo yao.
Mwanafunzi Walterblanca Mellows (kulia) wa shule ya   sekondari Canossa   iliyopo Tegeta jijini Dar-es-salaamani akitoa shukrani zake kwa uongozi wa kampuni  ya simu za mkononi ya Airtel mara baada ya
Airtel kuzindua programu  mpya   ya kuwawezesha wasichana wa shule za sekondari  kuweza kujiamini na kufanya maamuzi sahihi yatakayowafaa katika  kutimiza malengo yao kushoto ni Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Bi.Tunu Kivishe akifuatiwa na  Sigfrida  Mombo mwanafunzi wa kidato cha tatu na  Janeth Jareth mwanafunzi wa kidato cha pili.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari  Canossa, May Uisso(katikati) akijibu  swali mbele ya mkurugenzi wa huduma  kwa wateja Bi.AdrianaLyamba(kushoto) na Meneja wa huduma kwa jamii Bi. Tunu Kavishe (kushoto) wakati wa uzinduzi wa programu  mpya   ya kuwawezesha wasichana wa shule za sekondari  kuweza kujiamini na kufanya maamuzi sahihi yatakayowafaa katika  kutimiza malengo yao

Kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima Airtel Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo cha huduma Kwa jamii imezindua programu ya uwezeshaji kwa wasichana itakayo wawezesha wasichana wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 18 katika harakati za kufanikisha malengo yao ya baadae na kuwajengea uwezo wa kujiamini huku mafunzo hayo yakiwa yamebeba ujembe usemao “jenga maisha yako ya  baadae”

Akiongea wakati wa  ufunguzi wa Programu hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya wasichana  Canossa iliyopo Tegeta jijini Dar-es-Salaam Meneja Huduma kwa jamii Bi Tunu Kavishe alisema “Programu yetu ina lenga  kuwawezesha wasichana wote walioko shule za sekondari ikiwa ni muendelezo wa dhamira ‘Airtel Shule yetu’ ya kutoa elimu kwa jamii hasa   wasichana ili kuendeleza mahusiano yetu mazuri kati ya kampunina wateja wetu waaminifu.

Mbali na hayo ni ukweli kwamba wasichana wanahitaji sana uelewa wa kutosha pamoja na kutimiza malengo ili kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaifa au katika ramani ya dunia, Airtel inaamini wasichana hawa wanahitaji nafasi zaidi, mbali na masomo wanayosoma  wanatakiwa kujifunza mbinu mpya za maendeleo kutoka kwa wasichana wenzao na wakubwa ambao wamewazidi umri pia.

Nae,Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Kampuni ya Airtel Bi.Adriana Lyamba  ambae ndie aliyekuwa mtoa mada katika ufunguzi wa program hiyo kwa mara ya kwanza alisema  “najisikia fahari sana kwa Airtel kunipa nafasi ya kuwa mtoa mada wa kwanza mara baada ya ufunguzi wa program
hii ya kuwawezesha wanawake wenzangu katika shule za  sekondari ya wasichana ya Canossa.

Naiomba Airtel kuhakikisha programu hii itaendelea kwa shule nyingine za wasichana Tanzania na igusie mitaala mbali mbali ya uendelezaji wa taaluma kwa wasichana kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujiamini na kufanya maamuzi sahihi katika maisha.tutawaomba wafanyakazi wengine wa Airtel pamoja na wadau wetu katika biashara kujumuika nasi ili kuwaongezea na kuwapa wanafunzi uzoefu na mbinu mbalimbali  kwa kufanya hivyo itawaweze kuelewa ni jinsi gani wataweza kuchagua na kuendeleza taaaluma bora kwa maisha yao”.

“Kuna msemo unaosema kuwa ‘kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima’ kwahiyo tunaamini elimu mtakayotoa sasa  itakuwa chachu ya maendeleo kwa vizazi vijavyo” aliongeza Bi Adriana Tumejidhatiti kuisaidia jamii ya kitanzania,mbali na programu hii ya kuwawezesha wasichana  tumekuwa tukisaidia sekta ya elimu kupitia programu ya Shule Yetu kwa kugawa vitabu katika shule za sekondari nchini na nia yetu ni kuendeleza kiwango cha elimu kwa kuwezesha upatikanaji wa vitabu kwa urahisi zaidi kwa wanafunzai wa shule ya sekondari.tangu tulipoanza hii programu ya kusadia vitabu katiaka shule ya sekondari kwa miaka saba iliyopita  tumeweza kuwafikia zaidi ya sekondari 800 ambazo zipo nchi nzima.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU