Tuesday, March 13, 2012

AIRTEL YAJA NA INTERNET YA 3.75G KUTOA UBORA NA KASI ZAIDI KWA WATEJA.

Meneja Masoko wa Airtel Bw Salim Madati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya huduma mpya ya 3.75G katikati uzinduzi uliofanyika leo katika makao makuu ya Airtel Morocco ambapo sasa wateja wa Airtel wataweza kupata huduma ya internet iliyo ya kasi na kuwapatia ufanisi Zaidi katika shughuli zao za kila siku.
 Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor akionyesha jinsi gani huduma ya 3.75 inavyoweza kutoa huduma ya internet iliyo ya kasi na kuwawezesha wateja wa Airtel kufanya video call wakati wa  uzinduzi wa huduma ya 3.75 iliyofanyika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na waandishi wa habari , wakishuhudia (kulia) ni mkurungezi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya na (kushoto )ni Meneja masoko Salim Madati.
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa halfa fupi ya  uzinduzi wa huduma ya 3.75G  ambayo itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi  kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote. Uzinduzi huu ulifanyika katika makao makuu ya Airtel morocco
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor na mkurungezi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya  kwa pamoja wakionyesha jinsi gani huduma ya 3.75G  ilinavyoweza kuwawezesha wateja wa Airtel kupata huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet ikiwa ni pamoja na  kufanya video call wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa 3.75G  iliyofanyika makao makuu ya Airtel Morocco. 
Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangallor akiinua modem na kumkabidhi Mwandishi wa habari kutoka TBC Jane John aliyejishindia modem wakati wa uzinduzi wa huduma ya 3.75G iliyofanyika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wakishuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa Airtel
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma ya 3.75G uliofanyika leo katika makao makuu ya Airtel Morocco ambapo sasa wateja wa Airtel watapata internet yenye ubora na kasi  zaidi  , Pichani ni Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangallor

•       Airtel yajenga mtandao bora wa data barani Afrika

Uzinduzi wa Airtel 3.75G Tanzania utawapatia watumiaji  wa data huduma yenye kasi na ubora zaidi  katika simu zao
Kupitia internet ya 3.75 itawawezesha wateja kufanya maongezi ya simu ukiwa unamwona mtu, kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na kuperuzi na kupata miziki kutoka kwenye tovuti kupitia simu zao.

Jumanne 13 Machi 2011, Dar es Saalam–Airtel Tanzania leo imepiga hatua kubwa katika kujenga na kukuza mtandao wa technoloijia ya 3.75G Africa kwa  kuzindua rasmi  mtambo wa 3.75G nchini Tanzania,ambapo Airtel itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi  kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote.

Mkurungenzi Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangalloor alieleza” kukua kwa technolojia hii kutakuza ufanisi katika vyombo mbalimbali vya  mawasiliano (multimedia), kwa kuwa 3.75G itatoa internet yenye ubora na kasi  zaidi kwa  kuwezesha wateja kufungua tovuti mbalimbali, kufanya maongezi  ya simu kwa njia ya video , kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na pia  kupata muziki kutoka kwenye tovuti  kwa kutumia simu.

Teknologia ya 3.75G itatoa nafasi kwa wateja kupata mawasiliano ya data kwa njia tofauti na ya pekee kabisa, ndio maana leo Airtel tunajisikia fahari kuwa internet yetu ya 3.75G ni uvumbuzi na muendelezo wa mtandao (platform) wetu ili kuwawezesha wateja wa Airtel wote nchini kupata huduma ya internet au data yenye ubora wa hali ya juu pamoja na kasi zaidi”

Tunafanya ubunifu wa kuleta huduma zenye ubora zaidi katika mtandao kwa kuzingatia kuwa sasaivi dunia inauhitaji mkubwa sana wa huduma za kimtandao hasa kupitia simu ya mkononi.

Ukirejea takwimu zilizofanywa na kampuni ya McKinsey & Co. Telecommunications zinaonyesha  mpaka sasa kuna watumiaji wa simu za mkononi wapatao milioni 400 Afrika, na kwamba bara la  Afrika ni moja kati ya  soko linalokuwa kwa kasi zaidi huku soko la simu za mkononi likiendelea kukua na kupanuka zaidi na kufikia kutoa huduma za internet, huduma za benki kwa njia simu (mobile banking)   na biashara kwa njia ya mtandao yaani (mobile commerce) .

Hivyo basi kwa kuzingatia hili,  ndio maana Airtel tunaendelea na mikakati kama hii ya kuwaletea wateja internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ambayo ni sambamba  na lengo letu la kuendea kupanua mtandao ili kutoa mwanya wa mawasiliano kuwafikia wakazi wengi wa vijijini
ambao walikuwa wamesahaulika na mapinduzi ya mawasiliano katika bara la Afrika.

“wote tunafahamu kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya jamii ya sasa lakini bado kunachangamoto kubwa sana katika kupata huduma hii kwa baadhi ya sehemu barani Africa. Lakini tukumbuke Mawasiliano ni haki ya msingi kwa kila mtu na si vinginevyo hivyo kwa kupitia mtandao wa Airtel internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ninaamini tutaweza  kuunganisha idadi kubwa ya watu kwa kukuza mahusiano ndani na nje ya ya jamii zetu, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu, pamoja na kupanua wigo wa wale wanaofanya biashara kupitia mtandao wa internet “ Aliongeza Elangalloor.

Ikiwa tayari mteja ameunganishwa na teknologia ya 3.75G simu yake itaonyesha 3.75G, HSDPA, WCDMA or HSPA. Hii inategemeana  na Aina ya simu aliyonayo mtumiaji lakini kasi ya kuunganishwa ni yenye ubora zaidi.

Airtel itaendelea kuwekeza kwenye huduma ya data katika soko lake lote huku lengo likiwa ni kuwa mtandao mpana zaidi wa teknologia ya 3.75G katika bara zima, na itaendelea kutoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya watumiaji

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU