Thursday, March 8, 2012

BAADA YA UHARIBIFU WA VITI UWANJA WA TAIFA , WIZARA YA HABARI WATAKA KULIPWA

Waziri wa habari,vijana na utamaduni wa michezo 

Siku ya Jumapili Tarehe 04 Machi, 2012 kulikuwepo na Mchezo wa mpira wa miguu uliozikutanisha timu za SIMBA ya Tanzania na KIYOVU kutoka Rwanda, mchezo ambao ulifanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakati wa mapumziko ya mchezo huo, tulishuhudia kitendo kisicho cha kawaida kwa baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa mashabiki wa Klabu ya SIMA kuhama kwenye eneo walilokuwepo tangu mchezo ulipoanza na kwenda eneo walilokuwa wamekaa mashabiki wa Klabu ya YANGA na watazamaji wengine wa mpira wa miguu. Tukio hilo lilisababisha vurugu kubwa miongoni mwa washabiki hao na kuanza kuvunja na kurushiana viti. Tathimini ya uharibifu inaonyesha kuwa jumla ya viti 152 viliharibiwa na 11 vilivunjwa kabisa.

Wizara imesikitishwa na tukio hili lisilo la kistaarabu, na ambalo lingeweza kuleta maafa makubwa kwa wapenzi, washabiki waliohudhuria kwenye mchezo wa siku hiyo. Tukio hilo limeleta fedheha kwa Taifa letu.

Kutokana na uharibifu mkubwa uliofanyika, wizara inaingiza TFF Kulipa sh. Milioni tano (5,000,000/=) kwa ajili ya gharama ya matengenezo na urejeshaji wa viti vyote vilivyo haribiwa. Pamoja na hatua hiyo, TFF inaagizwa kuchunguza kwa kina na kuwachukulia hatua kali wote watakaobainika kuhusika na vurugu hizo. Endapo hali ya vurugu na uharibifu wa mali za uwanja zitaendelea wizara italazimika kufunga kwa muda matumizi ya uwanja huo.

Mwisho, natoa wito kwa wapenzi wote wa mpira wa miguu kuzishabikia timu zetu kwa amani na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani na usalama wa Watazamaji. Aidha, nawaomba wakati wote tufahamu kwamba ni wajibu wa kila mmoja wetu kulinda na kuutunza uwanja wa Taifa ili uendelee kuwa katika viwango vinavyokubalika Kimataifa na pia udumu kwa muda mrefu kwa manufaa ya Taifa letu.

IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU