Tuesday, March 6, 2012

UN YAENDESHA WARSHA KWA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI YA ZANZIBAR.

 Baadhi ya maafisa mawasiliano wakifuatilia kwa makini warsha iliyoandaliwa na UN
 Waziri wa nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dr. Mwinyihaji Makame akifungua warsha ya maafisa mawasiliano wa Wizara husika Zanzibar. Katikati ni kaimu mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Ruth Leano na kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alberic Kacou.

:Picha ya pamoja.
 
  Baadhi ya Wanamawasiliano wa serikali ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini warsha hiyo.
 Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu akiteta na Mheshimiwa Waziri Mwinyihaji Makame.
 Mmoja wa watoa mada kuhusu Mpango wa kufanya kazi pamoja kutoka UN Bwana George Otoo akiwasilisha maoni yake.
  Kaimu Mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Ruth Leano na  naye aliwakilisha program za UN zilizopo Zanzibar.
Mmoja wa Maafisa Mawasiliano toka serikali ya Zanzibar,Wizara ya Afya akisisitiza yaliyomo katika Mpnago wa Umoja wa Mataifa wa Msaada wa Mendeleo (UNDAP).


Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kupitia kundi la maafisa mawasiliano linalojulikana kama United Nations Communication Group (UNCG), limeendesha warsha ya siku moja mjini Zanzibar kwa maafisa mawasiliano wa serikali ya Zanzibar wanaofanya kazi katika wizara zote za Zanzibar. 

Warsha hiyo ilihudhuriwa na maafisa 40 wa wizara husika na ilihusu jinsi gani ya kuwawezesha wanamawasiliano wa serikali ya Zanzibar na UN kuimarisha mawasiliano yanayohusu maendeleo ya jamii, hususan ya Zanzibar.

 Mheshimiwa Dr. Mwinyihaji Makame, waziri wa nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar alifungua warsha hiyo. Julai 2011, UN pamoja na serikali ya Tanzania ilisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada wa Maendeleo wa miaka minne (UNDAP).

Mpango huu umelenga kufanya kazi kwa pamoja na serikali ya Tanzania. Utoaji wa warsha kwa maafisa Mawasiliano wa serikali ni moja ya mikakati ya kuimarisha utoaji taarifa wa maendeleo ya programu zinazofanywa kwa pamoja ambapo kundi la Mawasiliano la UN litakutana na wanamawasiliano wa bara mwezi ujao.
 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU