Tuesday, April 24, 2012

MWANARIADHA FABIAN JOSEPH KAFUNGIWA KUJIHUSISHA NA RIADHA

Mwana riadha Fabian Joseph.

Mwana riadha wa Timu ya Taifa Fabian Joseph amefungiwa kutoshiriki mashindano ya ndani na nje ya nchi mpaka mashindano ya olimpiki yatakapo malizika huko landan kutokana na utovu wa nidhamu. Mwanariadha huyo amefungiwa na kamati ya olimpiki Tanzania baada ya kushindwa kurejea katika kambi iliyopo Kibaha Mkoani Pwani inayojiandaa na mashindano ya olimpiki huko Landan. Mchezaji huyo baada ya kupigiwa simu na kocha wa timu ya riadha pamoja na katibu mkuu wa TOC hakupokea simu na viongozi hao kushindwa kuelewa anamatatizo gani.

Hivyo Katibu mkuu wa TOC Filbert Bayi alimtumia ujumbe wa meseji uliosomeka hivi :- BILASHAKA HUJAMBO NAKUANDIKIA HII MESEJI KAMA MZAZI, ULIONDOKA KAMBINI  TAREHE 09/04/2012 KWA RUHUSA KIPITIA FAMILIA, UKIWA NJIANI KWENDA KARATU KUSHIRIKI MBIO ZA NGORONGORO WEZAKO WOTE WALIOSHIRIKI KARATU WALIRUDI WOTE LAKINI WEWE HADI LEO TAREHE 19/04/2012 HUJARUDI KAMBINI NA UKIPIGIWA CM HUPOKEI, HIVYO NI NINI KAMA SIO UTOVU WA NIDHAMU?. UNAWEZA KUWA MKIMBIAJI MZURI NA BIGWA LAKINI BILA NIDHAMU UBINGWA WAKO HAUNA MAANA. POPOTE ULIPO UNATAKIWA UREJEE KAMBINI HARAKA, MARA YA PILI NTAKAPO WASILIANA NA WEWE SITAKUA KAMA MZAZI HAPO SASA NITAKUWA KAMA KATIBU MKUU WA TOC MWENYE MADARAKA YA KAMBI BAADA YA RT KUNIKABIDHI. Hiyo ni meseji ya Katibu mkuu kumtumia Fabian.

Majibu ya Fabian:- KILICHO NIFANYA NISIWEZE KUWASILI KAMBINI NI MTOTO WANGU ANAUMWA AKIPONA NITAKUJA NA KUPIGIWA SIMU NI JANA TU NILIKUTA GWANDU KANIPIGIA ILA KAMA NYIE MNAONA NI UTOVU WA NIDHAMU POA TU, MIMI NIFANYE NINI JUENI MIAKA YOTE NILIKUA MSTARI WA MBELE KUIWAKILISHA NCHI YANGU.

Kutokana na majibu ya mwanariadha huyo kamati ya ufundi ya TOC ilikutana tarehe 23/04/2012 na kutoa maamuzi hayo ya kumfungia mwanariadha huyo 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU