Friday, April 6, 2012

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA (TBF)


Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania TBF leo tarehe 06/04/2012 limapenda kuwajulisha Familia ya Mpira wa kikapu juu ya mambo matatu ya msingi ambayo yameamuliwa na Kikao cha Kamati ya Utendaji siku ya Tarehe 04/4/2012.
 
Ndugu zangu wanahabari kama mnakumbuka hivi karibu TBF ilitangaza kuufungia Mkoa wa Mwanza pamoja na Wachezaji wake walioshiriki ligi ya Taifa (TAIFA CUP) kwa kosa la kuvunja Kanuni za Mashindano na kudharau maamuzi ya Kamati za TBF.

Baada ya Taarifa hiyo kulikuwepo na majadiliano mbalimbali ya ndani ya Mkoa wa Mwanza pamoja na wadau wa familia ya Kikapu, na kutoa mawazo mbalimbali,MRBA baada ya kugundua kuwa walifanya kosa waliandika Barua kwa TBF yenye kuonyesha kukiri kosa, na kukubali kosa hilo lilisababishwa na Viongozi walioambatana na timu na kuwashawishi wachezaji wavunje kanuni za Mashindano.

Hivyo Kamati ya Utendaji ya TBF katika kikao chake imejadili barua yao kwa kina na kuamua ifuatavyo.
 
Adhabu inabaki kama ilivyo sasa kwa viongozi wa mkoa wa Mwanza kama zilivyoelekezwa na Kamati ya Utendaji ya TBF kwenye barua ya awali ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na shughuli zozote ambazo TBF itakuwa ikisimamia ama kuhusika kwa namna moja au nyingine kwa kipindi cha Mwaka mmoja. Viongozi hao ni wafuatao:

a. Kizito Bahati (Kaimu Mwenyekiti)
b. Robert Mwita (Kocha)
c. Amri Mohamed (Kocha Msaidizi)

Imeondoa adhabu kwa wachezaji wote wa mkoa wa Mwanza na wale waliohusishwa katika adhabu hii kwa kuwafungulia waendelee na shughuli zote za mchezo ndani na nje ya Tanzania kwa masharti ya kutojihusisha tena na matukio yoyote ya utovu wa nidhamu na uvunjifu wa amani katika michezo.

Imepunguza adhabu kwa mkoa wa Mwanza kwa kuufungulia kuendelea na shughuli zote za mpira wa kikapu nchini na nje ya nchi kwa sharti la kutojihusisha kwenye matukio mengine kama haya ama kushawishi au kuhusika kwa namna yoyote katika kuvuruga utaratibu utakaokuwa umekubalika.
 
Aidha, kwa kupunguziwa adhabu, Mkoa wa Mwanza pamoja na Wachezaji umeagizwa kulipa faini ya Shs. Laki tatu (300,000.00) kabla ya kuanza kushiriki katika shughuli zozote za mchezo wa mpira wa kikapu.Ndipo adhabu zitakuwa zimefutika.
 
Kamati ya Utendaji inautaka Mkoa wa Mwanza (MRBA) kuendelea kujitafakari katika nidhamu na uvunjifu wa amani ya mchezo na kuwataka viongozi watakao wajibika katika shughuli za kila siku kufuata utaratibu ulio sahihi katika kutekeleza wajibu wao.
 
Mwisho Kamati Utendaji inawataka viongozi waliotajwa hapo wazingatie adhabu hizo, yeyote atakae kwenda kinyume na maelekezo ya adhabu atua kali za kinidhamu zitachuliwa dhidi yake.
 
NBL:
Kamati ya Utendaji pia ilipitia maandalizi ya ligi ya Taifa Ngazi ya Vilabu ambayo imepangwa kufanyika tarehe 14/04/2012 hadi tarehe 21/04/2012 katika uwanja wa ndani wa Taifa.
 
TBF ilipokea barua kutoka Mkoa wa Dar es salaam (BD) yenye kuomba ushiriki wa timu sita kutoka katika ligi zao za wilaya ambazo wao wanazitambua kama Mikoa ya Kimichezo, ziweze kushiriki kwa maana ya mshindi wa kwanza na wa pili kutoka Mikoa hiyo mitatu ya Kinondoni ambapo kutakuwa na timu za Pazi na Oilers, Ilala Savio na Vijana na Temeke itawakilishwa na JKT na ABC.

Kamati ya utendaji imekubalina na ombi lao na tayari tumesha wajulisha,na taarifa zifika haraka kwa timu husika na kufuata taratibu kama zilivyo elekeza kwenye Kanuni za mashindano.

Mikoa Mingine ambayo tunategemea itashiriki ni pamoja na Tanga timu Mbili za Wanaume Bombo Giant na Tanga united na wanawake Tanga United Qeens ,Morogoro timu moja Mzinga Corporation , Dodoma timu moja ambayo ni Dodoma Spurs, Mbeya timu za Wanaume na Wanawake Mbeya flames (Mens) na Mbeya flames (Ladies) na Tabora timu moja ya Wanaume Center basketball Club.Hizo ndizo timu mpaka sasa ndio tunataarifa nazo.
U16 CLINIC ARUSHA:
Hivi karibu TBF ilipokea maombi ya Kocha msaidizi wa zamani wa New York knicks Greg Brittenham ambaye atakuwa na ziara ya kitalii ya kupanda Mlima Kilimanjaro mwishoni mwa mwezi wa tano na mara baada ya kumaliza kupanda angependa kubadilishana mambo ya kiufundi na familia ya Mpira wa Kikapu nchini, ikiwa ni pamoja na kuendesha mafunzo ya vijana wadogo walio chini ya miaka 16 kati ya tarehe 09/06/2012 na tarehe 10/06/2012 katika Mkoa wa Arusha .

TBF ipo katika mchakato wa maandalizi ya Clinic hiyo na inategema kutuma mwakilishi wake kwenda Arusha kuangali Mazingira ya Viwanja pamoja na kuanza kuwajulisha Walimu wa mashule kutayarisha vijana kwa ajili ya siku hiyo kwa Kushirikiana na Viongozi wa Mkoa wa Ausha wa Mpira wa kikapu jumla ya Vijana 100 tunategemea watashiri mafunzo hayo Wasichana 50 na Wavulana 50.

Gharama za Mafunzo hayo zinategemewa kufikia kiasi cha Tsh milioni Tano (5,000,000) tunakaribisha wadau mbali mbali wa Mkoa wa Arusha ni nafasi pekee ya kujitangaza kupitia vijana wadogo na kuonyesha uanamichezo katika kuwatia moyo vijana wetu.Kwa taarifa zaidi juu ya Greg na kupata wasifu wake unaweza tembelea http://www.nba.com/coachfile/greg_brittenham/index.html

 Mwisho tunapenda kuwaomba wadau mbalimbali waweze kujitokeza kuzisaidia timu zetu za Majiji ambazo zinatarajiwa kwenda nchini Uganda kwenye jiji la Kampala kwa ajili ya Michuano hiyo ya majiji sisi kama TBF tupo pamoja katika Harambee hiyo na kuendelea kutia mkazo kwa Viongozi wetu tukianzia kwa Mtsahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam na Majiji mengine ambayo yatashiriki pamoja na Wabunge wetu tunawaomba mzisaidie timu hizi.

 Asanteni kwa kutusikiliza tunawatakia Ijumaa kuu njema na heri ya Sikukuu ya Pasaka kwenu Waandishi wa Habari pamoja na Familia ya Mpira wa Kikapu Tanzania.

 Imetolewa na:
Michael Maluwe
Kaimu Katibu Mkuu (TBF)

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU