Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA) kimewateua maofisa watakaosimamia mpambano wa ubingwa wa Shirikisho hilo katika bara la Afrika(IBF Continental Africa Title) katika uzito wa Super Middleweight. Mpambano huoutafanyika tarehe 28 mwezi wa 4 katika ukumbi wa PTA jijini Dar-Es-Salaam.
Katika barua yake kwa promota wa mpambano huo bwana Lucas Munosi Rutainurwa wa kampuni maarufu yajijini Dar-Es-Salaam ya Kitwe General Traders Limited, Rais wa IBF/USBA DarylPeoples aliwataja maofisa hao kama John Shipanuka, Zambia (Refarii), WilliamSekeleti, Zambia (Jaji), Simon Katongole, Uganda (Jaji) na IsmaelSekisambu, Uganda(Jaji)
Msimamizi mkuu wampambano huo wa aiana yake ni Rais wa Shirikisho hilo katika bara la AfrikaOnesmo Ngowi toka nchini Tanzania . Aidha Ngowi pia ni Rais wa Kamisheni yaNgumi za Kilipwa nchini (TPBC) na Mkurugenzi wa Bodi ya Ngumi ya Baraza la Ngumila Jumuiya ya Madola (CBC).
Kuteuliwa kwa maofisahao kunazidisha hamasa wa mpambano huo ambao umekuwa ni gumzo katika viunga vyajiji la Dar-Es-Salaam pamoja na mikoa ya Morogoro, Tanga, Dodoma , Kilimanjaro,Arusha na Iringa.
Kufuatia na maelezo yapromota wa mpambano huo bwana Lucas Rutainurwa wa kampuni maarufu ya jijini Dar-Es-Salaamya ya Kitwe General Traders Limited mbali na pesa zampambano huo mshindi ataondoka na gari jipya lenye thamani ya shilingi milioni16.
Mpambano huu umeletahamasa kubwa nchini na kuanza kuwa kichocheo cha kuitangaza Tanzania katikamedani ya masumbwi ulimwenguni kwani mikanda ya IBF/USBA inaheshima ya kipekeekatika medani ya masumbwi duniani. Mbali na IBF/USBA mashirikisho au taasisinyingine zinazofuata nyayo ni pamoja na WBC, WBA na WBO.
Imetolewa na;
Onesmo A.M.Ngowi
IBF/USBA President for Africa
Director, Commonwealth (British Empire) Boxing Council (CBC)
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)
0 maoni:
Post a Comment