Sunday, April 29, 2012

TASWIRA ZA KILI MUSIC MKOANI DODOMA JANA

 Msanii wa kizazi kipya Diamond akiwa ameinuliwa juu na madansa wake katika onyesho la ziara ya washindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro lililofanyika juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
 Mshindi wa tuzo tatu za muziki za Kilimanjaro, Diamond akiwasalimia mashabiki wake kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma wakati wa onyesho la washindi wa tuzo za Kilimanjaro lililofanyika juiz Jumamosi.
  Nyota wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba, akitoa burudani pamoja na madansa wake kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma juzi Jumamosi wakati wa onyesho la washindi wa tuzo za Kilimanjaro
 Ommy Dimpoz akiwaimbia mashabiki wake wimbo wa Nai Nai, katika onyesho la washindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro katika onyesho lililofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
 :Madansa wa mwimbaji Ommy Dimpoz wakiweka mlango kwa ajili ya msanii huyo kupita ili kuweza kuwapa burudani wakazi wa Dodoma wakati wa onyesho la washindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri.
 Msanii wa muziki wa mduara akiwa stejini na shabiki yake wakipagawisha umati wa watu uliyofika kwenye uwanja wa Jamhuri kushuhudia onyesho la washindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro mwishoni mwa wiki hii.
 Barnaba akiwabembeleza mashabiki wa wa muziki wa Bongo Fleva Mjini Dodoma katika onyesho la vinara wa tuzo za muziki za Kilimanjaro lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa mpira wa miguu Jamhuri.
 Ben Pol akicheza na mshabiki wake jukwaani katika onyesho la vinara wa tuzo ambalo lilirindima mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
 Mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Kilimanjaro wa Mkoa wa Dodoma, Issa Kabuti akikamua kwenye onyesho la vinara wa tuzo, lililofanyika wa Jamhuri Dodoma.
 Mashabiki waliofika kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma kufutilia onyesho la vinara wa tuzo za muziki za Kilimanjaro, ambalo lilifanyika mwishoni mwa wiki.
 Kundi la mashabiki  walihudhuria onyesho la washindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro wakifutilia onyesho hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU