AfisaHabari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akisomahotuba kwa niaba ya Mshauri Mwandamizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwawa Mauaji ya KImbari nchini Rwanda, ambapo amehimiza nchi washiriki kuwa naimani na mahakama ya ICTR.
Wanafunzi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakisikiliza Lecture ya Profesa Chris Peter Maina wakati wa mjadala wawazi wa kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda Mwaka 1994.
Balozi Mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Sano Lambert akitoaneno la shukrani na pia kuasa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutetea amani namaendeleo kwa faida ya vizazi vijavyo na maendeleo ya ukanda wa Maziwa makuukwa ujumla.
Profesa Chris Peter Maina wa Kitivo cha Sheria cha ChuoKikuu cha Dar es Salaam akielezea na kufafanua umuhimu wa Mahakama, akitoleamfano ya ICTR kushirikiana na Taasisi na Mashirika ya Kijamii katikakuhakikisha haki inatendeka, haswa katika matukio kama ya uhalifu wa kivita.
Wanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichangia mada katika mjadala wawazi kuhusiana na madhara na nini tujifunze kutokana na mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.
Katibu Daraja la Kwanza wa Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania Bw. Ernest Bugingo akisisitiza jambo na kuwataka wanafunzi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujifunza zaidi na kusoma makala za mauaji ya Kimbari kupitia mtandao.
Wananchi wa Rwanda na Afrika Mashariki kwa Ujumla wametakiwakulinda na kudumisha amani katika eneo la maziwa makuu kwa kuwa hiyo ndiomisingi ya umoja na maendeleo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Msemaji na Mshauri Mwandamizi waKisheria wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari nchini RwandaBw. Roland Amoussouga, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC) Bi. Stella Vizo, amesema mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivitanchini Rwanda inasikitika na inatoa pole kwa wale walioathiririwa na vitavilivyotokea mwaka 1994na kuwa iko pamoja nao.
Aidha amesema tunapaswa kuweka kumbukumbu ya waliopotezamaisha na walionusurika , ambao kwa sasa wameathirika kimwili na kiakili.
Katika kongamano la kimataifa lililofanyika Chuo Kikuu chaDar es Salaam nchini Tanzania.
0 maoni:
Post a Comment