Thursday, May 24, 2012

EMAMANUEL TAGOE AVULIWA UBINGWA WA IBF

Shirikisho la Ngumi la Kitaifa bara la Afrika, mashariki ya kati na Ghuba yaUajemi (IBF) limetangaza kumvua ubingwa wa mabara katika uzito wa Junior Lightuliokuwa unashikiliwa na bondia Emmanuel Tagoe wa Ghana.

Katika kumvua ubingwa huo ambao Tagoe alikuwa autetee tarehe 26 May Rais waShirikisho hilo barani Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi bwanaOnesmo Ngowi alisema kuwa Tagoe anavuliwa ubingwa kutokana na kudanganya kwakekwenye vipimo vya afya!

Hii ni mara ya kwanza kwa Shirikisho hilo kumvua ubingwa bondia kwa madai yakudanyanya kwenye vipimo vya afya!

Bondia Emmanuel Tagoe alikuwa azipige na bondia Antonio De Vitis wa Italiakugombea ubingwa wa Junior Lightweight May 26, mwaka huu!

Msimamizi mkuu wa mpambano huo alikuwa Rais wa IBF katika bara la Afrika, Masharikiya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Ngowi pia ni Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania naMkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC).

Hii inawaweka mabondia wote katika hali ya hatari ya kuvuliwa ubingwa waoendapo tu wataonekana kuwa wamedanganya katika vipimo vya afya zao. Aidha,tabia ya mabondia wengi kutumia madawa ya kulevya inahatarisha ushiriki waokatika mchezo wa ngumi.

Katika msimamo wake huo Ngowi alisema kuwa ameuchukua uamuzi huo ili kutoafundisho kwa wale wote wanaofikiri kuwa udannganyifu hususan utumiaji wa madawaya kuongeza nguvu utawasaidia katika michezo.

Wanamichezo wanatakiwa wajue kuwa vipaji, juhudi za kufanya mazoezi na kujitumandivyo pekee vitakavyowapa ushindi katika michezo na sio dawa za kulevya.

Matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu yamepigwa marufuku hata michezo mbalimbalikama Olympic, World Cup na mashindano mengi ya ya kitaifa na kimataifa.

Hili ni fundisho rasmi kwa mabondia wa kitanzania wanaotumia madawa ya kulevyakama bangi na mengine ili washinde katika mapambano yao. Kwa kazi hii mchezoutabaki kwa wa wenye vipaji tu!

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU