KAMPUNI ya Bia yaSerengeti imetangaza kudhamini tuzo za Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2011kwa sh. Milioni 150, tuzo ambazo zinaandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habariza Michezo Tanzania (TASWA).Udhamini huo ulitangazwajana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti TeddyMapunda, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenyeklabu ya City Sports Lounge, Dar es Salaam, ambapo aliambatana na viongozi waTASWA.
Alisema kampuni yakeinaona fahari kuendelea kudhamini tuzo za TASWA ikiwa ni mwaka wa tatumfululizo, hivyo mwaka huu wameongeza udhamini zaidi ili kuzoboresha.
Alisema tuzo hizozitafanyika Juni 14 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee (VIP) Dar es Salaam nakwamba wana matumaini makubwa zitakuwa bora kuliko zilizopita.
Naye Mwenyekiti waTASWA, Juma Pinto aliwashukuru Serengeti na kusema udhamini huo ni ishara yanamna kampuni hiyo inavyothamini wanamichezo hapa nchini na kwamba umeongezekakwa kiasi kikubwa kutoka sh. Milioni 80 za mwaka jana.
Hata hivyo Pintoalisema milango ipo wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza kama wadhaminiwashiriki kwa
vile bajeti ya tuzohizo ambayo awali chama chake kimepanga ni sh. milioni 370, lakini hataudhamini huo unatosha kufanya kitu kizuri zaidi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TASWA, AmirMhando alisema Kamati Maalum ya Tuzo hizo inaendelea na mchakato wake wa kupatawanamichezo hao na kwamba kadri watakavyokuwa wanapiga hatua watatoa taarifakwa wanahabari.
Kwa miaka mitanoiliyopita walioshinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa TASWA walikuwa ni Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle (2007), Mary Naali (2008), ambaowote ni wanariadha, wakati 2009 na 2010 alikuwa mcheza netiboli MwanaidiHassan.





0 maoni:
Post a Comment