Tuesday, May 1, 2012

MABONDIA WAWILI WA TANZANIA WATINGA ROBO FAINALI

MABONDIA WAWILIWATANZANIA WATINGA HATUA YA ROBO KATIKA MASHINDANO YA KUFUZU  KUELEKEA OLIMPIKI YANAYOENDELEA CASSABLANCA MOROCCO.
Mobondia wa timu yataifa waTanzania Selemani Kidunda 69 kgswelter weight na Emillian Patrick 56kgs bantam weight wamesonga mbele katika mashindano ya kufuzu kuelekea katikakushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika London Uingereza,katikamashindano yaliyoanza tarehe 28/4-5/5/2012 Casablanca Morocco.

Mabondia hao wamefika hatua hiyo baada ya kushinda mapambanoyao ya awali kwa seleman Kidunda kumshinda Kab Thiam wa Senegal kwa RSC naEmillian Patrick kumshinda Tewodros Tilahun wa Ethiopia.

Mabondia hao sasa wamefika katika hatua ya robo fainaliambapo ni jumla wa mabondia nane waliofikia hatua hiyo na idadi inayotakiwakufuzu ni mabondia sita kwa kila uzito.

Mabondia hao kesho tarehe 2/5/2012 watapanda ulingoni kwaEmillian Patrick kucheza na Isaac Dogboe wa Ghana na Seleman Kidundaatacheza na Mehdi Khalsi wa Morocco .

Endapo watashinda watakuwa wameingia hatua ya nusu fainalina tayari watakuwa wamefikia hatua ya kupata medali ya shaba .

Tanzania ilipeleka jumla ya wachezaji wanne na viongoziwawili wachezaji wawili Victor Njaiti na Abdalah Kassim walitolewa katika hatuaza awali. viongozi walioambatana na timu ni Michael Changarawe na Remmy Ngabo.

Aidha kesho kutafanyika mkutano mkuu wa Shirikisho la ngumila Afrika (AFBC) Tanzania katika mkutano huo itawakilishwa na makamo wa Rais waBFT Michael Changarawe

Kwa niaba ya BFT tunawaomba watanzania wote kila mmoja kwaimani yake kuwaombea ili washinde na wafuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa kuzingatia kuwa kwa upande wa ngumitulishiriki olimpiki kwa mara ya mwisho mwaka 1996 Atlanta.

Makore Mashaga
Katibu Mkuu (BFT)

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU